Ushauri kuhusu machinga: TFF wapewe ofisi mjini, Karume pageuzwe kituo cha biashara

Ushauri kuhusu machinga: TFF wapewe ofisi mjini, Karume pageuzwe kituo cha biashara

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk.

Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
 
Machinga wameandaliwa eneo la kisasa na Wachina pale Ubungo.

Kutakuwa na vizimba 10,000
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk. Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Noted.
Hoja imeungwa mkono.
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk. Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Hata mimi nilifikiria hivi, TFF wahamishwe pale
 
Hapo kwenye TFF umefikiria vyedi kabisa
 
Haiwezekani machinga wote wa Dar es Salaam kuwarundika sehemu moja kama Karume! Hawa wachuuzi (not machinga) wanatokea sehemu mbalimbali za Dar es Salaam kila asubuhi na kurudi jioni kwenye makazi yao huko.

Busara kila Manispaaa (Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni, na Ubungo) iandae maeneo maalumu/masoko ikiwezekana kwenye kila Kata kwa ajili ya wachuuzi na wawe na vibali vya kufanya biashara kwenye maeneo hayo na wafanyie shughuli zao huko huko.

Kwenda mjini iwe ni kufuata mzigo na sio kutandaza bidhaa barabarani. Manispaa zi-encourage wafanyabiasahara wakubwa (wa Kariakoo na Posta) kufungua branches kwenye manispaa zao.

Wanaweza kwa mfano kuwapa viwanja bure au manispaa zikajenga na kuwapangisha kama motisha na hamasa ila mwisho wa siku watalipa kodi. Hii itasaidia kupunguza msururu wa wachuuzi kuelekea Kariakoo na Posta kila mara. Uholela ufike mwisho.
 
Ndio.

Ubungo itakuwa China ndogo.

Kariakoo itabaki kuwa historia.
Sahihi kabisa Kiongozi. Ubungo ambayo haina eneo la bahari ingetumia kuwepo kwake kama entry point ya Dar (lango la Jiji) kama fursa adhimu! Tatizo watendaji pale wamelala hakuna ubunifu. Wafanyabiashara wote kutoka mikoani na nchi jirani wangeanzia Ubungo and possibly kukamilisha mahitaji yao hapo hapo Ubungo.

Tatizo mfumo wetu wa kiserakali ni ule wa "nifanye, nisifanye mshahara uko pale pale" na pengine nikiwa mbunifu mwisho wa siku nitahamishiwa Nanyumbu kama "shukrani"! Why should I waste my time?
 
Ni wazo zuri but halita work ..

Kuna issue za demand na supply kwenye issue nzima ya biashara za wamachinga.

Hapo machinga complex wakirundikana wamachinga halafu demand ikiwa sio kubwa maana yake hujawasaidia wamachinga kwa sababu mapata ya biashara yatakuwa madogo
 
Back
Top Bottom