Ushauri kuhusu machinga: TFF wapewe ofisi mjini, Karume pageuzwe kituo cha biashara

Machinga wameandaliwa eneo la kisasa na Wachina pale Ubungo.

Kutakuwa na vizimba 10,000
Wamikoani nao wanaamishiwa Ubungo kwa wachina?

Hili haliwezi kuwa suluhisho la tatizo hili. Tunatakiwa kubadili vijana wetu kutoka kuwa wachuuzi wa bidhaa tena nyingi zikiwa fake (maana nyingine ukiziangalia kwa jicho la ukali zinavunjika!!!) kutoka nje ya nchi kuwa vijana wazalishaji mali na wauzaji wa mali hizo hapa nchini na nje ya nchi tena kwa faida. Hili ndilo suluhuisho la tatizo hili.

Hao wachumi na wataalamu wa fani mbalimbali waandae strategies za kuwezesha vijana kuzalisha mali na kuziuza nchini na ng'ambo. Uwezekano huo upo kwa sababu Mama 'kafungua' nchi, Mama 'katangaza' nchi, na Mama kapata 'msafisha taswira' ya nchi tena lobbyist nguli wa dunia.

Kwa hiyo hakuna kisingizio cha kushindwa kufanikiwa kuwasaidia vijana.
 
Haiwezekani machinga wote wa Dar es Salaam kuwarundika sehemu moja kama Karume! Hawa wachuuzi (not machinga) wanatokea sehemu mbalimbali za Dar es Salaam kila asubuhi na kurudi jioni kwenye makazi yao huko. Busara kila Manispaaa (Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni, na Ubungo) iandae maeneo maalumu/masoko ikiwezekana kwenye kila Kata kwa ajili ya wachuuzi na wawe na vibali vya kufanya biashara kwenye maeneo hayo na wafanyie shughuli zao huko huko.

Kwenda mjini iwe ni kufuata mzigo na sio kutandaza bidhaa barabarani. Manispaa zi-encourage wafanyabiasahara wakubwa (wa Kariakoo na Posta) kufungua branches kwenye manispaa zao. Wanaweza kwa mfano kuwapa viwanja bure au manispaa zikajenga na kuwapangisha kama motisha na hamasa ila mwisho wa siku watalipa kodi. Hii itasaidia kupunguza msururu wa wachuuzi kuelekea Kariakoo na Posta kila mara. Uholela ufike mwisho.
Hii ndy idea ya kisomi na endelevu...mimi nilikua nawaza tu.kwani mfano kama pale mbezi mwisho. Serikali Wakafanya analysis na kuwafidia watu nyumba kadhaa za kutosha..na wakawaondoa na kubadili use kuwa la wafanya biashara kulingana aina ya biashara .halafu wakawamwaga wamachinga eneo hilo na wakawachag ushuru endelevu kila mmoja kila siku mfn 1000.je hela waliowekeza on long-term basis je serkali itapata hasara?
Wamachinga wanafuata makutano ya watu sana. Mfano mbezi mwisho, mwenge, kariakoo etc. Hizi meeting point zote na zngnezo wakitengewa masoko watadhibitika kuliko hizi kelele zszokua na mwsho!!
 
Mvuto upi mkuu ! Hata kibaha kunaweza kuvutia kukuandalia na kupanga vyema!
... excellent! Lile pori la Kibaha panaweza kufunguliwa soko kubwa kabisa la bidhaa zinazoingia na kutoka badala malori kwenda hadi Kariakoo na Kigogo/Jangwani kila kitu kikaishia Kibaha. Ni thinking ndogo na ubunifu tu!
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk. Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani

mdukuzi sijakuzoea ukitoa point, hili wazo ni zuri mno mno
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk. Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Wazo zuri, hata hivyo Tff wamesha pewa eneo kigamboni ambako wanajenga kituo cha michezo, nadhani na ofisi zao wangezihamishia huko huko inge kuwa vizuri sana.
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk. Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Wazo zuri SANA

WATEKELEZAJI SASA
 
Haiwezekani machinga wote wa Dar es Salaam kuwarundika sehemu moja kama Karume! Hawa wachuuzi (not machinga) wanatokea sehemu mbalimbali za Dar es Salaam kila asubuhi na kurudi jioni kwenye makazi yao huko. Busara kila Manispaaa (Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni, na Ubungo) iandae maeneo maalumu/masoko ikiwezekana kwenye kila Kata kwa ajili ya wachuuzi na wawe na vibali vya kufanya biashara kwenye maeneo hayo na wafanyie shughuli zao huko huko.

Kwenda mjini iwe ni kufuata mzigo na sio kutandaza bidhaa barabarani. Manispaa zi-encourage wafanyabiasahara wakubwa (wa Kariakoo na Posta) kufungua branches kwenye manispaa zao. Wanaweza kwa mfano kuwapa viwanja bure au manispaa zikajenga na kuwapangisha kama motisha na hamasa ila mwisho wa siku watalipa kodi. Hii itasaidia kupunguza msururu wa wachuuzi kuelekea Kariakoo na Posta kila mara. Uholela ufike mwisho.
Umeleta suluhisho la uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI UJENZI AU SIJUI NI MAREKEBISHO SOKO LA KARIAKOO YATAANZA LINI?
... ningetamani libaki hivyo kama njia ya ku-encourage biashara kuhamia ngazi za manispaa badala ya kurundikana sehemu moja - Kariakoo. Kila manispaa iwe na soko lake kubwa la hadhi ya Kariakoo.
 
Kabisaa
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk.

Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Baada ya mwaka mmoja au miwili machinga watakuwa wameongezeka maeneo yale na mipango itabidi ibadilishwe upya.
 
Machinga wanategemea sana biadhaa feki, vitu vilivyoisha muda wake, vilivyoibiwa kutoka magodown, vilivyokwepa kodi hili kutoa nafuu kwa mteja. Wakipewa vizimba vya ukweli hawatokaa kwa kuwa wale watengenezaji bidhaa feki watawekwa wazi muno,watakaguliwa mara kwa mara. Solution sio kuwatafutia maeneo mapya hawataenda kwa kuwa wamezoea kukaba maduka ya wahalali ili kutoa punguzo ndio wauza. Kuendelea kuwatengea maeneo ni uhongo. Mfano machinga complex, bunju B walipewa soko wakaligomea, tegeta kwa ndevu wote waligoma kwenda nyuki. Wale wazee wa "atuchanjiiii"
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk.

Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Mkuu, hata ofisi za RC na DC Ilala nazo zingepaswa pia kuondolewa pale zilipo hivi sasa ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa kwa ajili ya wachuuzi wadogodogo.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi pale hapastahili kuwa ofisi za RC,posta majengo ya seeikali yamejaa popo
 
Baada ya serikali kuhamia Dodoma kuna majengo mengi sana kule posta hayana kazi mfano wizara ya afya , wizara ya ardhi, wizara ya fedha nk.

Serikali iwapatie TFF jengo mojawapo wafanye shughuli zao kama ofisi , wawapatie na ekari kadhaa za ardhi nje ya mji kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira, ule uwanja ugeuzwe kituo cha kibiashara kiunganishwe na machinga complex, machinga wa kariakoo wahamie Karume uwanjani
Wazo murua
 
Back
Top Bottom