Ushauri kuhusu machinga: TFF wapewe ofisi mjini, Karume pageuzwe kituo cha biashara

Machinga wameandaliwa eneo la kisasa na Wachina pale Ubungo.

Kutakuwa na vizimba 10,000
Wamikoani nao wanaamishiwa Ubungo kwa wachina?

Hili haliwezi kuwa suluhisho la tatizo hili. Tunatakiwa kubadili vijana wetu kutoka kuwa wachuuzi wa bidhaa tena nyingi zikiwa fake (maana nyingine ukiziangalia kwa jicho la ukali zinavunjika!!!) kutoka nje ya nchi kuwa vijana wazalishaji mali na wauzaji wa mali hizo hapa nchini na nje ya nchi tena kwa faida. Hili ndilo suluhuisho la tatizo hili.

Hao wachumi na wataalamu wa fani mbalimbali waandae strategies za kuwezesha vijana kuzalisha mali na kuziuza nchini na ng'ambo. Uwezekano huo upo kwa sababu Mama 'kafungua' nchi, Mama 'katangaza' nchi, na Mama kapata 'msafisha taswira' ya nchi tena lobbyist nguli wa dunia.

Kwa hiyo hakuna kisingizio cha kushindwa kufanikiwa kuwasaidia vijana.
 
Hii ndy idea ya kisomi na endelevu...mimi nilikua nawaza tu.kwani mfano kama pale mbezi mwisho. Serikali Wakafanya analysis na kuwafidia watu nyumba kadhaa za kutosha..na wakawaondoa na kubadili use kuwa la wafanya biashara kulingana aina ya biashara .halafu wakawamwaga wamachinga eneo hilo na wakawachag ushuru endelevu kila mmoja kila siku mfn 1000.je hela waliowekeza on long-term basis je serkali itapata hasara?
Wamachinga wanafuata makutano ya watu sana. Mfano mbezi mwisho, mwenge, kariakoo etc. Hizi meeting point zote na zngnezo wakitengewa masoko watadhibitika kuliko hizi kelele zszokua na mwsho!!
 
Mvuto upi mkuu ! Hata kibaha kunaweza kuvutia kukuandalia na kupanga vyema!
... excellent! Lile pori la Kibaha panaweza kufunguliwa soko kubwa kabisa la bidhaa zinazoingia na kutoka badala malori kwenda hadi Kariakoo na Kigogo/Jangwani kila kitu kikaishia Kibaha. Ni thinking ndogo na ubunifu tu!
 

mdukuzi sijakuzoea ukitoa point, hili wazo ni zuri mno mno
 
Wazo zuri, hata hivyo Tff wamesha pewa eneo kigamboni ambako wanajenga kituo cha michezo, nadhani na ofisi zao wangezihamishia huko huko inge kuwa vizuri sana.
 
Wazo zuri SANA

WATEKELEZAJI SASA
 
Umeleta suluhisho la uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI UJENZI AU SIJUI NI MAREKEBISHO SOKO LA KARIAKOO YATAANZA LINI?
... ningetamani libaki hivyo kama njia ya ku-encourage biashara kuhamia ngazi za manispaa badala ya kurundikana sehemu moja - Kariakoo. Kila manispaa iwe na soko lake kubwa la hadhi ya Kariakoo.
 
... ningetamani libaki hivyo kama njia ya ku-encourage biashara kuhamia ngazi za manispaa badala ya kurundikana sehemu moja - Kariakoo. Kila manispaa iwe na soko lake kubwa la hadhi ya Kariakoo.
Kabisaa
 
Baada ya mwaka mmoja au miwili machinga watakuwa wameongezeka maeneo yale na mipango itabidi ibadilishwe upya.
 
Machinga wanategemea sana biadhaa feki, vitu vilivyoisha muda wake, vilivyoibiwa kutoka magodown, vilivyokwepa kodi hili kutoa nafuu kwa mteja. Wakipewa vizimba vya ukweli hawatokaa kwa kuwa wale watengenezaji bidhaa feki watawekwa wazi muno,watakaguliwa mara kwa mara. Solution sio kuwatafutia maeneo mapya hawataenda kwa kuwa wamezoea kukaba maduka ya wahalali ili kutoa punguzo ndio wauza. Kuendelea kuwatengea maeneo ni uhongo. Mfano machinga complex, bunju B walipewa soko wakaligomea, tegeta kwa ndevu wote waligoma kwenda nyuki. Wale wazee wa "atuchanjiiii"
 
Mkuu, hata ofisi za RC na DC Ilala nazo zingepaswa pia kuondolewa pale zilipo hivi sasa ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa kwa ajili ya wachuuzi wadogodogo.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, hata ofisi za RC na DC Ilala nazo zingepaswa pia kuondolewa pale zilipo hivi sasa ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa kwa ajili ya wachuuzi wadogodogo.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Uko sahihi pale hapastahili kuwa ofisi za RC,posta majengo ya seeikali yamejaa popo
 
Wazo murua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…