USHAURI KUHUSU MAPATO YA TRA

dumesuruali

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2016
Posts
287
Reaction score
621
Habari za mchana wakuu...
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,,naomba nipate ushauri wenu kuhusu hili suala..

Nimemfungulia wife biashara ya vinywaji(soft drinks) kwa mtaji wa Tsh milioni mbili tu..

Sasa baada ya kwenda TRA kufanyiwa mkadirio wa mapato ameambiwa kwa kipindi cha mwezi wa saba(july 2019) mpaka mwezi wa kumi na mbili(december 2019) anatakiwa alipe Tsh 450,000/- ambapo kwa mwaka atatakiwa alipe Tsh 900,000/-

Hivi kweli biashara ya milioni mbili ulipie laki tisa kwa mwaka,,sasa hii ni biashara yetu au tunawafanyia biashara wao??

Nawasilisha..
 
mkuu hiyo kodi ni kubwa sana
kodi inatakiwa ilipwe kutokana na mauzo yako ,hebu jaibu kuonana na meneja wa kituo watakumalizia kamtaji kako, ila kama vp chukua kitambulisho cha machinga. Rais kasema mtaji wako kama ni chini ya milioni nne usisumbuliwee
machinga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Umezidi kihele hele

Ulifata nini TRA kwa uchuuzi wa 2M

Kwenye ku set charge ya huduma mbali mbali kuna somo la motive for the charged price

Kuna Charge zina lengo la kuongeza mapato na kuna charge za kupunguza foleni TRA

Kuna tozo zinawekwa kupunguza msongamano TRA
 
Unafanya kazi tra nini
 
Nafikiri wewe moja wapo ya watanzania wanaosabisha wafanyabiashara kufunga biashara zao
 
Soft drink anaenda TRA?
basi wewe ni tajiri maana unalipa Kodi ya Pango zaidi ya 200,000/
utalipa Service levy 120,000/ kwa mwaka Leseni 100.000/
kwa Kodi 900,000/ ni sawa kabisa kwani unaigawakatika awamu 4 kila baada ya miezi 3 apeleke 225,000/ na akizubaa ataambiwa anunue na mashine ya risiti 800,000/ kwani hawajui atakachokiuza huenda akauza soda za Jumla au kwenye Maharusi.
ACHANA na Leseni mfungulie km MAMA NTILIE tu hakuna watu wenye bahati ya kutokulipa kodi km wauza chakula/vinywaji na chingas
 
mkuu itapendeza kama ukinipa hilo darasa...
 

Sio mtaji wa chini ya 4mil ila ni MAUZO ya chini ya mil.4 ndio anatakiwa kupewa hio ID.
 
mkuu itapendeza kama ukinipa hilo darasa...


Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli amekwisha toa njia mbadala ya kusaidia ambayo ni vitambulisho vya Wamachinga kwa mtaji usiozidi 4M na wewe umesema una mtaji wa 2M

Mtumieni Dr Magufuli kabla hajaondoka nyie Wanyonge

Nawaambia Mtakuja kumkumbuka sana sana sana Mpendwa Dr Magufuli

Huenda huyu ndio Rais wa Mwisho kutoka kwny kundi la Walalahoi aliefanikiwa kupata Urais kutokana na vita vya Mabeberu wa Kisiasa hapa nchini
 
Ni mauzo yasiyozidi mil. 4 kwa mwaka na sio mtaji wa mil 4 kama unavyosema hapo juu.
 
Ni mauzo yasiyozidi mil. 4 kwa mwaka na sio mtaji wa mil 4 kama unavyosema hapo juu.


Assessments kiuhalisia hufanywa kwny mtaji sio mauzo kwa kuwa huwezi ku pre determine mauzo kwa uhakika
 
Assessments kiuhalisia hufanywa kwny mtaji sio mauzo kwa kuwa huwezi ku pre determine mauzo kwa uhakika
Kweli so huyu kodi ya TRA plus machine ya risiti haimusu zaidi ya leseni ya biashara na kitambulisho chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…