Ushauri kuhusu Mercedes Benz Salon car yenye CC 1790

Nokla

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
3,190
Reaction score
1,774
Wakuu nimevutiwa sana na hizi gari hasa yenye CC tajwa hapo juu, je ulaji wake wa mafuta ukoje, na upatikanaji wa spea na ukoje? technical problems, if any?

thanks

cc: Zanzibar Spices
 
Spare zake zipo chache na hivyo ni ghali. Na pia sio mafundi wengi wanaiweza hiyo gari. Maana kuna mshkaji wangu anayo inamsumbua sana.
 
boss,nunua hio gari. hio ni moja ya magari ya ulaya yaliyo rahisi kuyamiliki. spare zipo nyingi na mimi huwa nazileta kuna thread yangu humu na namba zangu zipo. nunua W203 from 2003-5 ni gari nzuri au kama bajeti inaruhusu nunua W204 from 2008
 
Spare zake zipo chache na hivyo ni ghali. Na pia sio mafundi wengi wanaiweza hiyo gari. Maana kuna mshkaji wangu anayo inamsumbua sana.

rafiki yako kakutana na wrong people,mafundi wazuri wapo na spare affordable zipo. nimekutag kwenye thread yangu kuhusu haya magari.
 
Hizo gari zinawazingua sana wenye nazo hasa vipuli na matengenezo kwa ujumla " kuwa makini.
 
Dah sasa jamani mnanichanganya, ninunue au nisinunue
 
....

cc: Zanzibar Spices

maana ya cc:.....
kwa kiswahili wanasema inaitwa nakala kwa: .....

Nilivyoelekezwa_ni kuwa ukiletewa barua na ukakutwa umewekwa kwenye kundi la cc:.... basi wewe unakuwa umepewa taarifa tu hautakiwi kuijibu bali anayetakiwa kuijibu ni yule mwenye anwani ya mtumiwa(receiver).

Sasa...ninauliza, je. Hapa JF kanuni ni hiyo hiyo ndiyo inayotumika wakati wa kutumia cc:.....?

Nimeuliza hili...maana matumizi ya cc:.....jukwaani yamekuwa mengi na nina wasiwasi watumiaji wake wanatofautiana kuhusu usahihi wa cc:....na hili laweza kuleta mtafaruku usiyo wa lazima.
 
Watu na maneno na story za vijiweni. Spea zipo nyingi tu. Na ukiweka spea leo hio hadi miaka mitatu au mitano kuibadili. Ila nashauri si kila fundi anajua mfumo ya hio gari. Natumia benz mwaka 6 sasa.
 
Mkuu hata me niungane na wanaosupport kukueleza uchague hilo gari. Achana na maneno ya watu, unapofikiria kununua kitu mkuu usitishike na maneno ya watu. Gari nunua sasa hivi kila kitu kinapatikana hapa town katika bei ya kawaida tuu bushlawyer
 
Last edited by a moderator:
maana ya cc:.....
kwa kiswahili wanasema inaitwa nakala kwa: .....

Nilivyoelekezwa_ni kuwa ukiletewa barua na ukakutwa umewekwa kwenye kundi la cc:.... basi wewe unakuwa umepewa taarifa tu hautakiwi kuijibu bali anayetakiwa kuijibu ni yule mwenye anwani ya mtumiwa(receiver).

Sasa...ninauliza, je. Hapa JF kanuni ni hiyo hiyo ndiyo inayotumika wakati wa kutumia cc:.....?

Nimeuliza hili...maana matumizi ya cc:.....jukwaani yamekuwa mengi na nina wasiwasi watumiaji wake wanatofautiana kuhusu usahihi wa cc:....na hili laweza kuleta mtafaruku usiyo wa lazima.

Sidhani hata kama wewe mwenyewe utakuwa umejielewa, ulichoandika
 
aisee, bado mnatuchanganya sasa, toeni mashule ya kueleweka basi
 
Mkuu nunua hizo gari especially kama uko Dar, kuhusu engine ziko mara mbili sikumbuki specs vizuri ila kuna mtu anayajua vizuri sana naweza kukupa namba yake PM.

Ila ukweli wa wazi ni kuwa spare haitaki hela ya mawazo hapo!!
"Germany techn. has never disappointed anybody so far"!!!!
 
maana ya cc:.....
kwa kiswahili wanasema inaitwa nakala kwa: .....

Nilivyoelekezwa_ni kuwa ukiletewa barua na ukakutwa umewekwa kwenye kundi la cc:.... basi wewe unakuwa umepewa taarifa tu hautakiwi kuijibu bali anayetakiwa kuijibu ni yule mwenye anwani ya mtumiwa(receiver).

Sasa...ninauliza, je. Hapa JF kanuni ni hiyo hiyo ndiyo inayotumika wakati wa kutumia cc:.....?

Nimeuliza hili...maana matumizi ya cc:.....jukwaani yamekuwa mengi na nina wasiwasi watumiaji wake wanatofautiana kuhusu usahihi wa cc:....na hili laweza kuleta mtafaruku usiyo wa lazima.

Wazo zuri mkuu ila ungekaa kwa pembeni kidogo maana hapa unaweza kupakwa grisi au oili wakakuharibia hiyo Van Heusen yako!!!
 
Mkuu nunua hizo gari especially kama uko Dar, kuhusu engine ziko mara mbili sikumbuki specs vizuri ila kuna mtu anayajua vizuri sana naweza kukupa namba yake PM.

Ila ukweli wa wazi ni kuwa spare haitaki hela ya mawazo hapo!!
"Germany techn. has never disappointed anybody so far"!!!!

Itakuwa poa sana mkuu
 
Back
Top Bottom