Ushauri kuhusu mtandao wa ttcl: Wired broadband

Ushauri kuhusu mtandao wa ttcl: Wired broadband

Mtu Mzima

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
394
Reaction score
124
Nina hitaji internet ambayo inaweza kuhimili kuendesha mkutano kwa njia ya video (Video conferencing) kwa ajili ya mikutano ya kikazi na watu ambao wapo nje ya nchi.

Kwa vile huwa napata shida sana na hii mitandao ya internet isiyotumia waya(3G) nimefikiria kujaribu intanet ya TTCL ya waya 6GB/mwezi ambayo inagharimu 70,000/- kwa mwezi + gharama za kuunganisha.

Kabla sijaingia gharama hizo ningependa kujua iwapo kuna mtu anatumia hizo huduma anipe uzoefu ili nisije kuingia mkenge.

Ninachojali zaidi ni kutokatika katika kwa mawasiliano hasa mchana wakati wa saa za kazi na uwezo wa kuwa na uhakika wa kasi ya kuteremsha angalau kwa 600kb/s mfululizo (kiwango cha chini).

Nitashukuru kwa kupata uzoefu wako na pia kama kuna mapendekezo mengine yanakaribishwa.

Asante
MM.
 
kama uko mwanza arusha au moshi chukua habari internet ya kasi na uhakika muzee
 
Nashukuru wote mlionipa ushauri hapa na pia kupitia PM.

Kwa wale mlionipa ushauri hapa:
Ndugu Lucasogutu na alikhalef, shughuli zangu nafanyia Dodoma, Iringa, Morogoro na Manyara.

Kuhusu mtandao wa wireless internet (3G) nimeshajaribu mitandao ya Voda, Zantel na airtel yote ni shida tupu hasa kati ya saa 4 asubuhi hadi saa 1 jioni.

Ndo maana nikafikiria kutoka nje ya hiyo ndoa.
Asanteni.
 
Zantel wana network 2. Kuna 3G pia wanayo cdma ambayo ipo speed also mordem zake hazitumii line
 
Kwa ulimwengu huu sishauri wired connection alternatives unaweza kwenda na wimax iko vizur sana japo cost itaongezeka kidogo
 
Alternative nyingine ni microwave, unaweza kutembelea website zoom tanzania upande wa telecom kuna kampuni zina enterprise solution nyingi
 
Back
Top Bottom