Mtu Mzima
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 394
- 124
Nina hitaji internet ambayo inaweza kuhimili kuendesha mkutano kwa njia ya video (Video conferencing) kwa ajili ya mikutano ya kikazi na watu ambao wapo nje ya nchi.
Kwa vile huwa napata shida sana na hii mitandao ya internet isiyotumia waya(3G) nimefikiria kujaribu intanet ya TTCL ya waya 6GB/mwezi ambayo inagharimu 70,000/- kwa mwezi + gharama za kuunganisha.
Kabla sijaingia gharama hizo ningependa kujua iwapo kuna mtu anatumia hizo huduma anipe uzoefu ili nisije kuingia mkenge.
Ninachojali zaidi ni kutokatika katika kwa mawasiliano hasa mchana wakati wa saa za kazi na uwezo wa kuwa na uhakika wa kasi ya kuteremsha angalau kwa 600kb/s mfululizo (kiwango cha chini).
Nitashukuru kwa kupata uzoefu wako na pia kama kuna mapendekezo mengine yanakaribishwa.
Asante
MM.