Ushauri kuhusu mtoto wangu, Mimi ni Mzazi mpya

Chocs

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
8,411
Reaction score
4,777
Habari zenu,

Nina mtoto wa kiume wa umri wa miezi mitatu na wiki mbili. Tangu nimejifungua sikupata maziwa siku tatu mfululizo kwahiyo alikuwa anapewa maji tu mpaka maziwa yalivyotoka.

Mtoto si mnyonyaji saana akinyonya titi moja basi lingine hataki mpaka wakati mwingine na nikimlazimisha anakua kama anataka kutapika, je ni kwamba bado hajaujua utamu wa nyonyo au ni uvivu? Hii imepelekea mimi kupunguza unywaji wa vitu vyepes kwani maziwa yanajaa sana nafanya kukamua namwaga

Wakati wa kulala nilishauriwa alale kwa tumbo.. Cha ajabu halali mda mrefu ila nikimlaza ubavu nakuta kajipindua kalala kwa mgongo ...kuna athari zozote juu ya hilo?

Tatu, hataki kubebwa kitoto toto wala kufunikwa mikono... Anapenda awekwe begani au aegemezwe kama anakaa, je ni wakati sahihi wa kukaa au umri bado?

Nne nahitaji kudhibiti tabia ya kunyonya kidole... Nitumie mbinu gani?

NB: Mimi ni mama mpya so nina meengi ya kujifunza kuhusu watoto.

KARIBUNI KWA USHAURI
 
1. Si lazima mtoto anyoye matiti yote mawili kwa wakati mmoja, kama kashiba kwa titi moja basi muache usimlazimishe kunyoya la pili.

2. Watoto wengi katika umri huo hulala kwa mgongo sijui ni nani aliyekushauri umlaze kwa tumbo, anyway ngoja wengine waje.

3. Kama mtoto anayonya na kushiba sidhani kama kuna haja ya kumzuia kunyonya vidole, mwache anyonye lkn kama kweli hutaki basi nenda maduka ya vifaa vya watoto kuna plastic za kufunika vidole kuzuia asivinyonye.

Nihayo tu
 
Asante kwa ushauri... Well,n nmtoa huduma wangu ndo alinisisitiza kumlaza mtoto kwa tumbo kwani atalala kwa muda mrefu soon after kukauka vizuri na kufunga kwa kitovu

Nilijaribu pacifier akaikataa, nimeachana nayo nitajaribu hicho kidude cha plastic
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwanza nikupongeze sana kwa kujifungua salama usalimini..

1...kuhusu kunyonya watoto wanajua shibe zao so akinyonya hilo titi moja mwenyewe anakua ameshiba plz usimlazimishe anyonye yote Mawili

2...kama una maziwa mengi kuna njia za kuhifadhi kwa matumizi ya baadae,yakamue yanaweza kukaa wiki 1 katika friji Miezi 6 kwenye freezer..

3...kuhusu ulalaji sio lazma alale unavyotaka wewe mwenyewe yupo comfortable na anavyolala ila akiwa awake mlaze kitumbo tumbo ili mishipa ya kichwa ikaze (tummy time)...

4..unyonyaji wa kidole kama huupendi akiweka kidole mdomoni we mtoe hivyo hivyo hadi ataacha hii ime work sana kwa binti yangu

Halafu hako kajamaa kanaonekana kamekaza sana very strong lol.
 
Hellow Chocs,

Hongera sana kwa kujifungua.Nitaweka nyongeza tu kwasababu wenzangu wameshachangia mengine na sina ya kusema zaidi ya haya.
Kitaalamu mtoto aliye chini ya miezi minne hashauriwi kulazwa na tumbo hasa kama mzazi hayupo karibu kumtazama.Inasemekana mishipa ya shingo inakuwa haijakazana kwahio anaweza ashindwe kujigeuza na akose pumzi na kupeleka kifo hii imeshafanyiwa uchunguzi na imetokea sana.Mtoto aliye na umri wa chini ya miezi minne anashauriwa kulazwa ubavu au chali.Ushauri wa farkhina ni mzuri mlaze kifudifudi ukiwepo karibu ili kufanya mazoezi lakini isiwe njia ya kumlaza mtoto kabla hujapata uhakika anaweza kujigeuza shingo.
Mtoto wa miezi mitatu kubebwa kama anakaa i guess si tatizo kwasababu kawaida mtoto anaanza kukaa kuanzia miezi 4 lakini again bado mishipa ya shingo haijazakazana sawasawa haishauriwi sana mbebe kama kwa mbele usimuweke kiunoni.
Kila la kheri kumlea mwanetu
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kwa kupata mtoto.....
Watoto wanaonyonya vidole huwa wanakuwa wavivu sana kunyonya na hata kula, wanapokua. Na pia wanakuwa siyo wasumbufu, wapo comfortable na vidole vyao. kumdhibiti kuwa inakuwa ngumu kidogo.
Ulalaji wa tumbo huwa tunashauriwa sababu watoto huwa wana tabia ya kucheua. sasa wanapokuwa usingizini na kama kalala kwa kutumia mgongo ni rahisi sana akicheua anashindwa kuyatoa, but akilalia tumbo na akacheua basi utakuta yamemwagikia kwenye kitanda. ni kwa ajili ya tahadhari tu na si kingine.
Kila la heri katika malezi mapya
 
Asante sana
Nimekuelewa
 
Asante dadake mimi

Na kweli ni mvivu sijui tukianza chakula mbadala Itakuwaje

Miss u
 
Hellow Chocs,

Hongera sana kwa kujifungua.Nitaweka nyongeza tu kwasababu wenzangu wameshachangia mengine na sina ya kusema zaidi ya haya.
Kitaalamu mtoto aliye chini ya miezi minne hashauriwi kulazwa na tumbo hasa kama mzazi hayupo karibu kumtazama.Inasemekana mishipa ya shingo inakuwa haijakazana kwahio anaweza ashindwe kujigeuza na akose pumzi na kupeleka kifo hii imeshafanyiwa uchunguzi na imetokea sana.Mtoto aliye na umri wa chini ya miezi minne anashauriwa kulazwa ubavu au chali.Ushauri wa farkhina ni mzuri mlaze kifudifudi ukiwepo karibu ili kufanya mazoezi lakini isiwe njia ya kumlaza mtoto kabla hujapata uhakika anaweza kujigeuza shingo.
Mtoto wa miezi mitatu kubebwa kama anakaa i guess si tatizo kwasababu kawaida mtoto anaanza kukaa kuanzia miezi 4 lakini again bado mishipa ya shingo haijazakazana sawasawa haishauriwi sana mbebe kama kwa mbele usimuweke kiunoni.
Kila la kheri kumlea mwanetu

Kweli maisha ni kujifunza pia kutoka kwa wengine
Asante mpnz
Be blessed
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana Chocs kama alivyosema Fixed Point watoto wa umri huo hucheua sana hasa mara baaya kunyonya hivyo hushauriwa kulazwa kifudifudi ili akicheua na labda mtu wa kumsafisha yuko mbali basi asimeze na labda kupaliwa au hata kuingia puani na hivyo kumuweka mtoto katika hali ya hatari na hilo la kulala kwa muda mrefu kama kalalia tumbo nalo ni kweli, ila kama mwenyewe au mtu unayemuamini yuko karibu basi hakuna tatizo la kumlaza chali. Pia ukishamnyonyesha mweke begani na unakuwa kama unamfanyia massage mgongoni taratibu mpaka atoe burps kati ya mbili au hata tatu husaidia kuhakikisha motto asicheue mara kwa mara.
 
Maelezo yenu yamenitoa shaka kwani na mimi mtoto wangu ndio kwanza ana miezi mitatu na wiki mbili. Tatizo lake anapenda kulalia tumbo.hapendi kubebwa kitoto na anapenda awekwe kitako.yeye shingo yake imekaza tangu akiwa na miezi miwili na hata ukimbeba unajua kuwa shingo yake imekaza kwani halegezi kichwa na amekaza kweli kweli. Tatizo moja tu nimeshindwa kulizuia. Anapenda kunyonya kidole na ukimlaza anaviringika kitanda chote.
 
2. Watoto wengi katika umri huo hulala kwa mgongo sijui ni nani aliyekushauri umlaze kwa tumbo, anyway ngoja wengine waje.

Kwa kawaida huwa inashauriwa mtoto alazwe kwa mgongo na hii ni kwa sababu ya kiusalama ili isiwe rahisi kwa mtoto kujiziba pua na kupelekea kifo...

Kulazwa kwa tumbo ni kitu cha kawaida na hushauriwa hivi ili kuruhusu mtoto atoe gesi kwa urahisi tumboni (kucheua)...

Mtoto mwenye kukosa kucheua/kujaa gesi tumboni huwa analia sana na hukataa chakula/maziwa au kunyonya...

Onyo:
Mtoto anayelazwa kwa tumbo inabidi awepo muangalizi ili isijetokea mtoto akajiziba pua kwa kuilalia au kujifunika na nguo/shuka.
 
Tangu nimejifungua sikupata maziwa siku tatu mfululizo kwahiyo alikuwa anapewa maji tu mpaka maziwa yalivyotoka.

Kwanza hongera sana shemkwe sikujua kumbe umekuwa mama sasa eenh...

Duh!! Nimejikuta nashangaa hapo kwenye kupewa maji mtoto mdogo wa masiku kadhaa...very strange na si nzuri kitabibu....

Kwa wenzetu waliondelea huwa mtoto anapewa 'donors milk' au 'newborn formulas' hadi mama atapoanza kutoa maziwa vizuri...

Mtoto si mnyonyaji saana akinyonya titi moja basi lingine hataki mpaka wakati mwingine na nikimlazimisha anakua kama anataka kutapika, je ni kwamba bado hajaujua utamu wa nyonyo au ni uvivu?

Watoto wa kiume si wavivu kula, huyu bwana mdogo mbona awa hivyo tena!!!

Je unapomaliza kumnyonyesha huwa unamuweka begani na kumpiga piga, papasa mgongo wake ili acheue?

Mtoto asipocheua huwa analia na unapomlazimisha zaidi kula huwa anatapika...

Hii imepelekea mimi kupunguza unywaji wa vitu vyepes kwani maziwa yanajaa sana nafanya kukamua namwaga

Kama unaona bado anakuwa mbishi kunyonya basi unaweza yakamua maziwa na kuhifadhi kwa jokofu...

Then uwe wampatia kwa chupa, huenda akakubali kunywa kwa chupa...

Maziwa ndani ya jokofu hukaa siku 5 kabla ya kuwa spoilled...na kama ukiyafreeze yanakaa muda mrefu zaidi maana huweza kukaa hadi miezi 5...

Tatu, hataki kubebwa kitoto toto wala kufunikwa mikono...

Hili lisikupe tabu, huenda anataka kuwa huru hivyo alivyo...

...au aegemezwe kama anakaa, je ni wakati sahihi wa kukaa au umri bado?

Si wakati sahihi wa kukaa...

Isipokuwa unaweza kumuegemeza katika namna ambayo ni nusu kulala nusu kukaa...

Nne nahitaji kudhibiti tabia ya kunyonya kidole... Nitumie mbinu gani?

Umejaribu kutumia 'pacifier'?
 
Hongera sana Chocs kama alivyosema Fixed Point watoto wa umri huo hucheua sana hasa mara baaya kunyonya hivyo hushauriwa kulazwa kifudifudi ili akicheua na labda mtu wa kumsafisha yuko mbali basi asimeze na labda kupaliwa au hata kuingia puani na hivyo kumuweka mtoto katika hali ya hatari na hilo la kulala kwa muda mrefu kama kalalia tumbo nalo ni kweli, ila kama mwenyewe au mtu unayemuamini yuko karibu basi hakuna tatizo la kumlaza chali. Pia ukishamnyonyesha mweke begani na unakuwa kama unamfanyia massage mgongoni taratibu mpaka atoe burps kati ya mbili au hata tatu husaidia kuhakikisha motto asicheue mara kwa mara.

Asante BAK

Hua namuweka begani na anacheua mara mbili mpaka tatu

Kuna muda akicheua yanatoka mpaka na puani
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Maelezo yenu yamenitoa shaka kwani na mimi mtoto wangu ndio kwanza ana miezi mitatu na wiki mbili. Tatizo lake anapenda kulalia tumbo.hapendi kubebwa kitoto na anapenda awekwe kitako.yeye shingo yake imekaza tangu akiwa na miezi miwili na hata ukimbeba unajua kuwa shingo yake imekaza kwani halegezi kichwa na amekaza kweli kweli. Tatizo moja tu nimeshindwa kulizuia. Anapenda kunyonya kidole na ukimlaza anaviringika kitanda chote.

Hua najiuliza watoto wanaizaliwa sana miaka hii Kwanin wananyonya vidole?
 
Back
Top Bottom