Ushauri kuhusu mtoto wangu, Mimi ni Mzazi mpya

Ushauri kuhusu mtoto wangu, Mimi ni Mzazi mpya

Kwanza hongera sana shemkwe sikujua kumbe umekuwa mama sasa eenh...

Duh!! Nimejikuta nashangaa hapo kwenye kupewa maji mtoto mdogo wa masiku kadhaa...very strange na si nzuri kitabibu....

Kwa wenzetu waliondelea huwa mtoto anapewa 'donors milk' au 'newborn formulas' hadi mama atapoanza kutoa maziwa vizuri...



Watoto wa kiume si wavivu kula, huyu bwana mdogo mbona awa hivyo tena!!!

Je unapomaliza kumnyonyesha huwa unamuweka begani na kumpiga piga, papasa mgongo wake ili acheue?

Mtoto asipocheua huwa analia na unapomlazimisha zaidi kula huwa anatapika...



Kama unaona bado anakuwa mbishi kunyonya basi unaweza yakamua maziwa na kuhifadhi kwa jokofu...

Then uwe wampatia kwa chupa, huenda akakubali kunywa kwa chupa...

Maziwa ndani ya jokofu hukaa siku 5 kabla ya kuwa spoilled...na kama ukiyafreeze yanakaa muda mrefu zaidi maana huweza kukaa hadi miezi 5...



Hili lisikupe tabu, huenda anataka kuwa huru hivyo alivyo...



Si wakati sahihi wa kukaa...

Isipokuwa unaweza kumuegemeza katika namna ambayo ni nusu kulala nusu kukaa...



Umejaribu kutumia 'pacifier'?

Asante shemkwe... za masiku tele?

Hua namuweka begani na anacheua bila tatizo

Chupa Nilijaribu kumpa nayo ila anang'ta tu ile chuchu na havuti ng'o

Pacifier nayo Nilijaribu akaigomea, nikiweka kinywani tu anaitema

Nilipewa maj fulani iv katika chupa... Ladha yake ina sukari kwa mbaali...Yani km maziwa iv

Now ana 4 months nimeanza kuona kasi ya kunyonya
 
Hongera sana Chocs kama alivyosema Fixed Point watoto wa umri huo hucheua sana hasa mara baaya kunyonya hivyo hushauriwa kulazwa kifudifudi ili akicheua na labda mtu wa kumsafisha yuko mbali basi asimeze na labda kupaliwa au hata kuingia puani na hivyo kumuweka mtoto katika hali ya hatari na hilo la kulala kwa muda mrefu kama kalalia tumbo nalo ni kweli, ila kama mwenyewe au mtu unayemuamini yuko karibu basi hakuna tatizo la kumlaza chali. Pia ukishamnyonyesha mweke begani na unakuwa kama unamfanyia massage mgongoni taratibu mpaka atoe burps kati ya mbili au hata tatu husaidia kuhakikisha motto asicheue mara kwa mara.
hongera baba BAK
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom