Ushauri kuhusu ng'ombe

larryone30

New Member
Joined
May 6, 2019
Posts
4
Reaction score
2
Habari wa ndugu

Mimi nimfugaji wa ng'ombe, jana ng'ombe alizaa ndama bila hata msaada wowote yaani kusaidiwa kuvuta ndama, na tayari kondo limetoka.

Leo nimerudi kazini nimekuta ng'ombe(mama) amelala chini tu, nimejaribu kumshtua aamke ameshindwa lakini anajitahidi kutaka kuamka.

Naomba ushauri nifanye nini maana daktari anayemtibu simpati kwenye simu.

Naombeni mnisaidie huduma ya kwanza.
 
Ungeandika upo wapi, number zako za simu ungepata msaada kirahsi
 
Inaweza ikawa milk fever, husababishwabna upungufu was calcium mwlini hutikea Mara nyingi pindi ng'ombe anapo jifungua mtafte ntaaramu was mifuge ata kusaidi ng'ombe wako ata simama
 
Niliwahi kusikia ng'ombe akishazaa kondo lake litolewe karibu naye mapema kwamba anaweza kulila/kulilamba/kunusa na kumletea madhara....ulihakikisha hajaligusa kondo lake?
 
Huenda ngombe wako alilamba kondo,, jitahid ngombe wako akikaribia kuzaa uwepo karibu.

Mtafute mtaalamu wa mifugo ngombe wako atainuka tu ,madini ya calcium yamepungua

Babu yangu aliniambia ng'ombe akilamba lamba kondo anaishiwa nguvu ya kusimama na madini ya kalishiamu

Mimi sio daktari ni uzoefu wangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…