Ushauri kuhusu Nissan Dualis

Ushauri kuhusu Nissan Dualis

.
BM824378_54b294.jpg
 
IDFakenyingine nunua gari ukifuata sana ushauri wa humu hutonunua cha msingi fuata ushauri wa yule aliesema anayo huu mwaka wa nne.

Cha kuongezea zingatia sana vilainishi ambavyo manufacturer amependekeza. Usije sikiliza ule ushauri wa ...hii oil unaweka gari yeyote ni sijui ni malaya so haina shida aisee don't go that way utalia

Kila la kheri kwenye mchakato!! Sema nini watu wananunua mandinga kila leo mazee nchi imefunguliwa hii [emoji23][emoji23]
 
Bila kuwachosha, niende kwenye mada.

Nimetokea kuipenda sana hii gari, na ninataka kuinunua.

Lakini kabla 'sijajilipua', ningeomba mawili matatu kuhusiana nayo kutoka kwa wataalam wa magari au watu waliowahi kumiliki Nissan Dualis.

Je, ni kweli ENGINE na GEARBOX za hii gari ni PASUA KICHWA SANA..?!

Vipi uhimilivu wake kwenye ROUGH ROADS..?
Manake ITAPAMBANA na kilometa 25 za rough road kabla ya kugusa lami mara 3 kwa wiki!

Vijiweni maneno ni mengi, nimekuja humu nakiamini kuna WAJUZI na WATAALAM!

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Cc: Extrovert RRONDO Offshore Seamen JituMirabaMinne Boeing 747 chilubi

Mimi sina info sana kuhusu hii gari. Labda wenye experience zao wazishare hapa.
 
Shukrani.
Mchango wako ni wa thamani kubwa sana.

Vp na yenyewe ina sensors kama zote..?

Kama inazo, ni zipi hasa zinazoleta misala ya ghafla barabarani ili mtu ujiandae?
Gari kama hiyo tena imeanza kuzalishwa 2007, sensors kama zote ni kitu cha kawaida.

Kwani sensor zina ubaya gani mkuu. Kukujulisha matatizo yaliyopo kwenye gari yako ndio ubaya?

Halafu engine ya Cc2000 bila hizo sensors ungekuwa mafuta lita 1 unaenda hata 3km hadi 5. Isingenunulika.
 
Hakuna gari hapo,kama una pesa ya kutosha nunua subaru forester hutojutia kabisa
Kati ya Subaru yenye TURBO na isiyo na Turbo, ipi ungemshauri mtu ambaye speed siyo priority bali fuel economy ndo priority yake?
 
IDFakenyingine nunua gari ukifuata sana ushauri wa humu hutonunua cha msingi fuata ushauri wa yule aliesema anayo huu mwaka wa nne.

Cha kuongezea zingatia sana vilainishi ambavyo manufacturer amependekeza. Usije sikiliza ule ushauri wa ...hii oil unaweka gari yeyote ni sijui ni malaya so haina shida aisee don't go that way utalia

Kila la kheri kwenye mchakato!! Sema nini watu wananunua mandinga kila leo mazee nchi imefunguliwa hii [emoji23][emoji23]
Ni kweli ulichoandika.

Kuna watu ukitaja tu Nissan, tayari wanaanza kusagia!

Lkn mara nyingi hawana sababu za kitaalam.

Binafsi, kwa sasa natumia Toyota... lakini Nafsi yangu inazikubali sana gari za Nissan! [emoji1]
 
Gari kama hiyo tena imeanza kuzalishwa 2007, sensors kama zote ni kitu cha kawaida.

Kwani sensor zina ubaya gani mkuu. Kukujulisha matatizo yaliyopo kwenye gari yako ndio ubaya?

Halafu engine ya Cc2000 bila hizo sensors ungekuwa mafuta lita 1 unaenda hata 3km hadi 5. Isingenunulika.
Mkuu hujakutana na wale wa kukwambia Nissan ina sensors za kuzima gari ghafla barabarani ikinyeshewa na mvua..?! [emoji1][emoji1][emoji1]

Hao ndo wanatuvuruga! [emoji1]
 
Hii gari ni nzuri na ipo comfortable, na hata kwenye njia mbovu inapita.
Sema kikubwa ni service, usizidishe mda. Na unapofanya service uwepo kumsimamia fundi.

Kwa upande wangu nilipata taarifa za kimakosa mtandaoni kuwa usibadilishe engine oil mpaka rangi ibadilike, hii ilifanya niue engine, na ikabidi kwenda kuweka engine nyingine na ninaifanyia service ndani ya mda na haijasumbua hadi leo. (Engine ikifa sikushauri kufanya overhaul, chukua fundi wako unayemwamini katafute engine nyingine)

Cha msingi weka recomended oils, kwenye engine oil 5w30 ndo nzuri, usije kumsikiliza fundi anakuambia sijui SAE-40 au nyingineyo.

Kingine jiandae kwa gharama ya spare zake, zipo juu kidogo, ila ukiweka unasahau.

Shida yake nyingine ni vitambaa vya kwenye paa na milango kutoka, ili wapo wanaorudishia.

Vitu vingine nilivyowahi kubadilisha tangia nianze kuitumia; (Inaenda miaka miwili sasa)
1. CV Joint na rubber boot
2. Brake pads
3. Sensor ya ABS
4. Bushes
 
Mbina husem mambo mengine ya ndan zaud kuhusu hii gar?
Eg. Ukipata matatizo ukataka kuiuza Resale Value yake ipo chini hivyo kuuzika nako inasumbua bciz watu wanhofu na kampun ya Nissan.
Nimeshuhudia moja imeuzwa hapa kitaa chetu kwa 10M na modelbya 2008
 
Ulishaona gari ina muonekano mzuri, iko comfortable halafu wamiliki wake wanakimbilia kutaka kuiuza haraka haraka, tena kwa bei ndogo, basi wewe jua tu kuna kitu hakiko sawa kiuchumi kuhusu hiyo gari.
Hizi hapa chini ni mojawapo ya gari zenye hiyo tabia.
1. Nissan Dualis
2. Nissan Xtrail
3. BMW
 
Tz tuna umaskini sana hakuna gari mbaya kikubwa service hizo subaru unazoshauriwa kununua nazo zinahitaji service kwa wakati ww ukiona mtu anahoji sana kwenye kutaka kununua chuma bas hana hela na ushauri ni kwamba bora atumie usafiri wa uma binafsi hatoweza
 
Bila kuwachosha, niende kwenye mada.

Nimetokea kuipenda sana hii gari, na ninataka kuinunua.

Lakini kabla 'sijajilipua', ningeomba mawili matatu kuhusiana nayo kutoka kwa wataalam wa magari au watu waliowahi kumiliki Nissan Dualis.

Je, ni kweli ENGINE na GEARBOX za hii gari ni PASUA KICHWA SANA..?!

Vipi uhimilivu wake kwenye ROUGH ROADS..?
Manake ITAPAMBANA na kilometa 25 za rough road kabla ya kugusa lami mara 3 kwa wiki!

Vijiweni maneno ni mengi, nimekuja humu nakiamini kuna WAJUZI na WATAALAM!

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Cc: Extrovert RRONDO Offshore Seamen JituMirabaMinne Boeing 747 chilubi
Nenda kwenye page za hawa Samatimemagari. Wanakuwa maelezo ya magari mengi yanayotumika Tanzania. Unachagua mtandao wa kusoma taarifa. Mimi napendelea kuwasoma twitter
 
Hizo ndo zenyewe sasa hata haugusi miaka kumi Wewe ushazoea zile kila km3000 unabadili huku siyo. Ni km 200,000 plus ndo unabadili
Gari gani hio ya Kubadilisha gearbox oil kila km 3,000?
 
Gari nzuri hautojutia. Sasa kilometers 25 za rough road wewe unaishije huko halafu upeleke gari kama hii huko?! Huko kuna gari zake. Hii gari haitaki mikiki ya makusudi.

Kwa dharula haina shida ila kama unataka kuisumbua kwa makusudi utakutana na gharam za service.

Kuhusu gear box na engine sio kweli. Hii gari ipo vema sana tu. Shida ni watu kuchanganya oili kuweka oil tofauti ya zile pendekezwa.

Hii gari ina oil yake special ambayo inawekwa kwenye gear box na special ya engine na zina nembo ya kampuni ya Nissan kabisa.

Sasa wengi wanaoziita mbovu sijui pasua kichwa. Mawili. Amenunua kwa mtu ambaye aliikosea adabu au yeye mwenyewe alikuwa hayupo makini ndio imemharibikia.

Ila yote kwa yote ni gari nzuri. Nadhani inafanya vema sana kimauzo zimenunuliwa sana kipindi hiki yaani katika gari utakutana nazo sana barabarani ni hii Nissan Dualis, IST, Subaru Forester XT kwa kutaja chache.
 
Back
Top Bottom