Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Ndugu zangu,
Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu, nimegundua kwamba kila ukitokea msiba mkubwa wa kiongozi au mtu mwenye ushawishi mkubwa katika jamii, kumekuwa na wimbi la nyimbo nyingi zinazotungwa ili kuomboleza na kumkumbuka mwendazake.
Kwa kweli wasanii huwa wanajituma sana kipindi kama hicho, wengi wakiona ni fursa kubwa ya kusikika na kuonekana kwa sababu jamii nzima inakuwa katika mjadala juu ya msiba huo. Nakumbuka kipindi cha kifo cha Nyerere, kulikuwa na wimbo mmoja uliitwa 'Nenda Mwalimu', ulichota sana hisia za Watanzania wengi.
Sasa ninachoona ni kuwa, kwanza hatuna utaratibu mzuri wa kuzitunza na kuzihifadhi nyimbo hizo. Nadhani tunaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kuzitambua, kuzikusanya na kuzihifadhi nyimbo hizo.
Lakini ushauri wangu mwingine mkubwa zaidi ni huu. Kwa nini kusiwe na utaratibu maalumu wa Wasanii, labda wakishirikiana na Kamati ya Taifa ya Maafa ili nyimbo hizi zinapotolewa, Wananchi wawe wanazinunua kwa njia ya mitandao, yaani kwa kudownload na kulipia kiasi kidogo cha fedha. Pia makampuni ya Video na Television nayo yahamasishwe katika zoezi hili ili kulipa zoezi hili mwamko zaidi. Fedha zitakazokusanywa zinaweza kuwa zinapelekwa katika mfuko maalumu unaohusiana na shughuli aliyokuwa anafanya Marehemu au mambo yale ambayo Marehemu yalikuwa yanamgusa zaidi.