waheshimiwa
naomba ushauri
nataka ninunue solar kwa ajili ya nyumba yangu ya vumba 4
matumizi yangu ya awali ni: Friji, pasi, tv, radio, taaa,
sijavuta bado umeme wa Tanesco lakini nataka nianze na hiyo solar
je nahitaji kuwa na bajeti ya kiasi gani?
je mnaweza kunshauri ninunue solar ya aina gani kwa matumizi hayo
je mnaweza kunshauri kampuni zipi zinaweza kunipa huduma bora zaidi
mambo yakiwa supa bas hamna shaka naweza kuongeza solar ya kupasha maji moto ya kuoga (lakini kwa sasa hiyo haipo kwenye mahesabu
mkuu kwenye solar .. jaribu kuondoa wazo la pasi na friji kwanza coz vitu hivi vinakula umeme sana.
labda wakati unaitafuta uzungumze na mtoa huduma kuhusu uwezekano wa kupata pasi na friji inayotumia solar..
matumizi ya kawaida kama taa, kuchaji simu, tv, radio, laptop n.k utaenjoy.
Bajeti kias gan inahitajika?
neggirl
wasikutishe mkuu,Bajeti kias gan inahitajika?
neggirl
wasikutishe mkuu,
chukua watt300 kwa gharama ya laki350 chkua betri kubwa kwa gharama ya laki3, chkua inverter kwa laki moja na chkua charger controller kwa elf90, utakuwa umeshamaliza kuhusu umeme kinachobaki ni nyaya, taa, cable, nk kulingana na mahitaji yako.
Mkuu hiyo watt 300 ndo itaweza kuwasha vitu vyote alivyodai anataka atumie? Pasi, fridge pamoja na taa!
Nimekuwa na swali hilohilo.
Si kweli kwamba ataweza kuwasha hivyo vitu vyake vyote kwa hiyo 300 Watts. Inverter haiwezi kutoa umeme zaidi ya ule ulioingizwa kwa battery (uliojazwa na solar pannel), pia solar pannel haiwezi/ haziwezi kujaza battery zilizo kubwa kuliko uwezo wake.
Ushauri wa kutumia vitu vya solar kama fridge na tv ni mzuri ILA bei za fridge ya solar ni kichaa, labda kama kuna mtu anajua mahali wanapouza chini ya 1.5m (tena fridhe ndogo).
Kupasha moto maji ni rahisi, tunatumia "solar heat"; Yaani moto wa jua moja kwa moja na hiyo unanunua solar water heater inayofanya hivyo. ziko water heater za namna mbalimbali yakiwemo majiko.
Simple calculations;
Mahitaji ya kawaida ya nyumba ni (Ukitoa pasi na jiko)
1. Tv, Deki na decorder-150 Watts
2. Taa 10 - 50 Watts
Kwa haraka hiyo ni 200 Watts ukiongeza 50% unakuwa safe kwa matumizi ya masaa 8 hivi.
So kwa haraka unapata 300 Watts kama alivyosema mdau mmoja hapo juu ILA huwezi kuwasha (PASI Wala JIKO)-Yaani ukibadili umeme kwenda joto unatumia nishati nyingi sana. Mfano, Jiko Wattage zikiwa chache sana ni 2000Watts (Sahani moja) na Pasi zinaanzia 1000Watts, vifaa hivi pekee vinatupa 3000Watts ambayo ni mara kumi ya mahitaji ya kuwasha taa na tv.