Ushauri kuhusu Toyota Old School

Ushauri kuhusu Toyota Old School

ubwindo

Member
Joined
Jul 23, 2017
Posts
43
Reaction score
29
Habari wakuu.
Kwanza nikiri wazi kwamba mimi ni mpenzi mkubwa sana wa magari ya zamani.

Yaani nikiyaona barabarani huwa napagwa hasa likiwa bado kwenye hali nzuri kimuonekano na kwa imani yangu nahisi huwa yako imara sana.

Nimeunga unga na sasa nahitaji nichkue gari aina ya Toyota model za tourer chaser, avante, cresta na nyinginezo.

Sina ujuzi hata kidogo wa magari na ndio maana nimekuja hapa kuomba maoni yenu mbalimbali wadau kuhusu upatatikaji wake (mkononi), bei zake zikoje, matumizi ya mafuta yakoje, gharama za utunzaji na vipuri vyake n.k

Asanteni.
 
Asilimia kubwa Toyota za old ni nzuri ila zinatofautiana kwenye maswala ya mafuta, mfano hizo ulizotaja mafuta inabidi uwe sawa kidogo...ukitaka zenye nafuu nenda katika koo za Corona, Carina, Corolla, Premio nk.
 
Back
Top Bottom