1.Kama unaenda na ndege, Panda ndege inayo enda msumbiji pemba air port. Ndege hiyo inaitwa LAM. Kama haipo ulizia yoyote inayoenda Pemba ya msumbiji. Ukishuka apo, ulizia gari za kwenda montopwezi, ukishazi panda omba kushukia sehemu moja inayo itwa NANYUPU. Hapa ndo chimbo lipo haswaaa. Uko montopwezi ni makazi na mjini. Kumbuka msumbiji wanaongea kireno .ukiwa pemba unaweza ukapata bahati ukakutana na mtanzania au usipate mpaka utakapo fika montopwezi-Nanyupu. Hivyo ukifika air port. Mwambie mtu yeyote kwa kireno kwamba unaitaji kwenda kituo chadaladala za kwenda montopwezi) Unaweza kusema hivi (stoapidiri, miamostra, e aonde na paraji di shapa di montopwezi) yaani ninaomba, unionyeshe ni wapi kituo (paraji) cha daladala (shapa) za montopwezi. Watakuonyesha. Hayo maneno nimeyaandikwa kwa Kiswahili hili upate kuyasoma vizuri. Ukisha panda hiyo shapa(daladala) mwambie konda akushushe nanyupu. Mwambie hivi kobura doli Nanyupu paraji. Yaani konda nanyupu shusha . Ukishashuka hutaona tofauti ya Tanzania wabongo ni wengi kaka..KWA BASI2.Panda gari mpaka mtwara-ukifika mtwara itakuwa ni jioni. Chukua guest house yoyote ila ukilala guest ya kilindima mtwara inaweza kuwa vizuri zaidi kwasbb watu wanao enda msumbiji ulala pale, so unaweza kupata kampani3.Asubuhi utapanda gari za kwenda boda, daladala zinapaki apo, nauli ni shs 5000 mpaka boda. kumbuka kupitia emigiration4.Ukifika boda panda mtumbwi kuvuta mto Ruvuma nauli ni shilling 5000-10000 ya Tanzania. Kabla haujapanda mtumbwi ulizia kama pantoni inafanya kazi. Kama inafanya kazi tumia pantone kuvuka nauli ni shs 500tshs na ni salama.5.Ukisha vuka tayari utakuwa msumbiji upande wa pili, hivyo utapanda gari zingine mpaka MSIMBWA.kumbaka ukisha vuka utatakiwa kugonga passport kwa emigration. Kumbuka msumbiji kila sehemu wanakagua vitambulisho vya taifa au passport.6.Ukifika MSIMBWA unaweza kupata bahati ukakuta gari ndogo private inaenda montopwezi ukapanda. Kama hutaipata, utatakiwa kulala msimbwa mpaka kesho yake asubuh, na utapanda gari zinazoenda montopwezi. Kama hazipo, utapanda gari zinazoenda NAMPULA then utaomba kushukia MITORO.7.Ukiwa mitoro utaziona dala dala nyingi zinaenda montopwezi. Kumbuka ukitumia njia ya basi, kokote utakapo pita watu wanaongea Kiswahili hivyo hutapata shida sana. Msimbwa kuna kabila ya wamwani wanajua Kiswahili kabisa. Nauli ya kutoka mtoni mpaka MSIMBWANI 350mitikashi sawa na 18-20elf ya tshs. Kutoka Msimbwa mpaka Montopwezi andaa kama 500mitikashi ila haitaisha ni sawa na 25-26elf ya tshs.Ziponjia nyingi ila soma hiyo kwanza ukiitaji nyingine nitakwambia mkuu. MUNGU WETU NA AKUTANGULIE NA KUKUFANIKISHA