BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Wadau naomba ushauri maana naelekea kuwa confused.
Nina mtoto mwenye umri wa miaka 7. Huyu mtoto amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuumwa tumbo kwa style ya kushtukiza, yaani inamuanza ghafla na baada ya muda fulani anapata nafuu. Nimejaribu kwenda hospitali mbali mbali, lakini wamekuwa wakipima magonjwa ya tumbo, typhoid, malaria, urine etc. bila mafanikio yoyote.
Hivi karibuni doctor akaniambia inaweza kuwa hernia, kwani kila kipimo tulichopima hapakuwa na ugonjwa wowote.
Dalili:
Anapatwa na maumivu kwenye sehemu ya kitovu na juu ya kitovu. Mara nyingi humtokea usiku na asubuhi.
Miaka miwili iliyopita alikuwa akiishi mikoa yenye joto hapakuwa na tatizo lolote. Ila sasa tuko mikoa yenye baridi ndo tatizo limekuwa serious.
Naombeni ushauri, nimetafuta taarifa nyingi sana kuhusu ugonjwa huu kwa madaktari, kwenye vitabu, internet na social media mbalimbali. Wengine wanasema nitumie dawa za asili, wengine wanasema afanyiwe upasuaji, wengine wanasema dawa za asili ni kwa ajili ya kutuliza maumivu, sasa nitumie ushauri gani?
Nimetumia dawa nyingi sana lakini mwanangu haponi.