Ushauri kuhusu Umbilical Hernia kwa mtoto wa miaka 7

Ushauri kuhusu Umbilical Hernia kwa mtoto wa miaka 7

BASHADA

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
513
Reaction score
148
Wadau naomba ushauri maana naelekea kuwa confused.

Nina mtoto mwenye umri wa miaka 7. Huyu mtoto amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuumwa tumbo kwa style ya kushtukiza, yaani inamuanza ghafla na baada ya muda fulani anapata nafuu. Nimejaribu kwenda hospitali mbali mbali, lakini wamekuwa wakipima magonjwa ya tumbo, typhoid, malaria, urine etc. bila mafanikio yoyote.
Hivi karibuni doctor akaniambia inaweza kuwa hernia, kwani kila kipimo tulichopima hapakuwa na ugonjwa wowote.

Dalili:
Anapatwa na maumivu kwenye sehemu ya kitovu na juu ya kitovu. Mara nyingi humtokea usiku na asubuhi.
Miaka miwili iliyopita alikuwa akiishi mikoa yenye joto hapakuwa na tatizo lolote. Ila sasa tuko mikoa yenye baridi ndo tatizo limekuwa serious.

Naombeni ushauri, nimetafuta taarifa nyingi sana kuhusu ugonjwa huu kwa madaktari, kwenye vitabu, internet na social media mbalimbali. Wengine wanasema nitumie dawa za asili, wengine wanasema afanyiwe upasuaji, wengine wanasema dawa za asili ni kwa ajili ya kutuliza maumivu, sasa nitumie ushauri gani?
Nimetumia dawa nyingi sana lakini mwanangu haponi.
 
Ukujibiwa hili nitakuwa nimepata ufumbuzi
 
Mkuu The secretary, na wewe una tatizo kama langu?
Naona wadau wamegoma kutusaidia.
 
Last edited by a moderator:
kwa mimi niliona mtu aliyepata tatizo hilo alikuwa msichana alifanyiwa operation na mpaka sasa asumbuliwi tena ila yeye alikuwa mkubwa sijajua kwa mtoto.ngoja tusubiri wadau
 
Sio Dr, Nadhani ni Appendesite!(sijui km inaandukwa hivyo) Nilikuwa na tatizo hilo hasa wakati wa baridi au mawingu ya mvua tumbo maeneo hayo nilikuwa na maumivu makali!
 
Sio Dr, Nadhani ni Appendesite!(sijui km inaandukwa hivyo) Nilikuwa na tatizo hilo hasa wakati wa baridi au mawingu ya mvua tumbo maeneo hayo nilikuwa na maumivu makali!

ulitumia dawa gani?
 
[h=2]Pole sana Bashada. Kama mtoto ana Umbilical Hernia, basi hilo si tatizo kubwa. Nenda hospitali wakamfanyie Ultra Sound ili kudhibitisha kama kweli ni Umbilical Hernia. Mimi mwanangu alisumbuliwa sana na tatizo hilo haswa anapokuwa sehemu ya baridi. Kwa sasa ni kijana mkubwa na anasoma Chuo Kikuu cha Mzumbe college ya Mbeya. Akiwa huko mwezi May mwaka huu aliumwa sana, nafikiri kutokana na baridi ya huko. Ilibidi arudi nyumbani kwa matibabu. Nilikwenda Aghakan hosp na katika kuongea ongea na baadhi ya wagonjwa pale walinishauri nimuone Dr. mmoja anaitwa Tumaini Njau. Huyu Dr. anafanya pale Aghakan na part time anafanyia Mbweni Hosp. kwa masista. Nilipoonana naye alinishauri nimpeleke kijana wangu Mbweni Hosp na atakuja kumfanyia operation huko. Sababu kubwa ya kumpeleka Mbweni hosp ni gharama kubwa sana za pale Aghakan.
[/h]Tulikwenda Mbweni hosp na Dr. Tumaini Njau akamfanyia hiyo operation na ikawa very successful. Tena bahati mbaya zaidi mwanangu alikuwa na Double Umbilical Hernia, lakini kwa utaalamu wa huyo Dr. kila kitu kilienda vizuri kabisa na alilazwa kwa siku moja tu, tukaruhusiwa kurudi nyumbani. Mimi nakushauri uende Mbweni hosp mtoto akafanyiwe vipimo. Ikibainika ni Umbilical Hernia omba afanyiwe operation na Dr. Tumaini Njau. Gharama haitazidi 300,000/=.

Ukionana private na Dr. Njau gharama zitakuwa juu zaidi hata kufikia 1,000,000/=. Na pia ukienda Aghakan gharama hazitapungua 3,000,000/=. Wewe nenda Mbweni hosp kwa masista kama mgonjwa wa kawaida, chukua vipimo then majibu yakitoka toa ombi la kufanyiwa operation na Dr. Tumaini. Ni operation ndogo tu maybe kama ya appendix. Dr. Tumaini surgeon mzuri sana na ana utaalamu wa kuifanya vizuri na isirudi tena kwa kuweka mesh ya kuzuia ku-reoccur. Wengine huwa wanafanya bila kuweka mesh na matokeo yake hiyo hernia inarudi tena. Kama unahitaji msaada zaidi ni PM. All the best na mpe mtoto pole.
 
hicho ni kitovu tu kitaisha taratibu wakati wa ukuaji

Kama ni Umbilical Hernia haiwezi kuisha hata ufanyeje. Dawa ni operation ya kuiondoa tu. Mimi nilipiga chenga kwa mwanangu tangu akiwa na umri wa miaka minne, lakini nimekuja kusalimu amri akiwa na miaka 22. Asikudanganye mtu eti ni kitovu kitaisha kadiri anavyokua. Utakuwa unamtesa mtoto tu kama nilivyofanya mimi.
 
Asilimia kubwa (75%) umbilical hernia kwa watoto zinaziba by the age of 5 years, zilizobaki huhitaji operation ya kuziba. Zenye shida ni zile ambazo shimo ni dogo, kwa kuwa utumbo hujikita na kusababisha maumivu makali ya mara kwa mara. Muone daktari kwa maoni zaidi
 
Back
Top Bottom