TDibwe
Member
- Oct 20, 2023
- 81
- 96
IPO taasisi inaweza tumika kama msambazaji wa vitu unavyouza.na kupokea pesa wakati mteja anapoenda kupokea alichonunua mkoani popote Tanzania.hii taasisis yenyewe kufanya E Commerce,Sheria zake zinakinzana,ila mtu/Kampuni binafsi inaweza tumia miundo mbinu yake kusambaza na kupokea malipo kuktumia miundombinu yake.System ya E Commerce ni $35,000.Habari wanabodi,
Shida ya hii forum unaweza kuomba ushauti mijitu inakutazama tu[emoji706]
Twende kwenye Mada
TZ na dunia nzima wafanyabiashara na wanunuzi wanakutana na barrier ya uaminifu.Hasa wanunuzi waliombali na muuzaji lets say mikoa tofauti.
Kwa kuona hiyo.Ndipo zinakuta technology ya Ecommerce.Zipo site nyingi za Ecommerce kama ebay,Amazom,Alibaba,kikuu, na nyingine nyingi.
Kupitia hizi ecommerce maarufu mnunuzi anaweza kununua kitu chochote akiwa sehemu yoyote ile duniani.
TOFAUTI na hizo ecommerce kubwa yani International kuna hizi za local kama Jiji, jumia, Kupatana.com hizi site na App zinatofauti kidogo kwani hutaweza kufanya malipo ya bidhaa moja kwa moja badala yake utawekewa namba ya muuzaji.
SASA WAZO NDIO LINAKUJA HAPO
Nini kinakwamisha ecommerce za bongo kutokuwa na payment gateway?
Na uzuri wake ni kwamba kwa kila bidhaa itayouzwa unakata % kadhaa.Mfano bidhaa inauzwa 10,000 tsh/ wewe unakata 500/ na mteja atakapo fanya malipo unaweka malipo PENDING..mteja atakapothibitisha kapokea malipo ndio nawewe unaruhusu malipo kwa muuzaji ndivyo wengine kina Amazon hufanya hivyo kuepusha wizi!!?
Sasa kwa uelewa wako hapa bongo ugumu utakuja wapi kwenye kutengeneza mfumo kama huu wa kuuza na kununua.Wewe unakuwa kama mtu wa kati tu unaemuunganisha mnunuzi na muuzaji
Sidhani kama nimeeleweka kwakua nimeandika kwa spidi ya jet bila kufanya marejeo ya bandiko ila kama umepata concept karibu tujadili.
Karibu