Ushauri: Kujenga nyumba mjini au nje ya mji

Jenga nje ya mji , hewa safi nk ...mimi najipanga nijenge Kisongo, Arusha nikinunua na Toyota crown hybrid ya 2021 na Mitsubishi outlander yangu ya 2018 itatosha...ndoto za kununua apartment Masaki au Upanga zimeyeyuka

Tena nitalima na bustani ili Nile mbogamboga fresh kabisa na nitafuga kuku wa kienyeji
 
[emoji16]Kwakweli....hapo maisha burdani,weekend unachoma zako mbuzi kwenye bustani yako.
 
Jenga mjini kisha baadae jenga huko nje ya mji. Kwa nini nasema hivyo, hizo sehemu zote ni zako ila huko nje ya mji kwa kuwa kutakugharimu mafuta au nauli pamoja na kukosa huduma muhimu za kijamii ujenge baadae. Hii ya mjini unaweza kuijenga na kuanza kuishi mpk hapo baadae ukaenda huko nje ya mji kufanya maisha ya ndoto yako
 
Yah nadhani inaweza kuwa option nzuri kwa sasa,nafikilia kuanza kujenga mjini kwa muundo wa nyumba ya kupangisha, na huko nnje ya mji ndio nitajenga "dream house" [emoji4]
 
Jenga mjini achana na huko mapolini utakuwa bored sanaa ,
 
Inategemeana na mji uliopo

Kuna miji inakua kwa kasi sana, ukijenga pembezoni, ndani ya miaka kama mitano hivi panakuwa pashachangamka

Ila kuna miji hususani mikoani, ukuaji uko slow sana
So ukijenga inachukua muda mrefu sana kuchangamka

Na kwa mikoani tatizo jingine pembezoni mwa miji utakutana na wenyeji wa asili wa maeneo hayo

So kuna namna ya maisha yatakutesa sana hasa unapoishi na watu wa jamii moja

Ila binafsi napenda kukaa pembezoni, kuna uhuru mkubwa japo changamoto nazo ni lukuki...
 
Pia mifano yenu iseme nje ya mji ni wapi kwa sababu kuna mjini vijiji vipo karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…