Ushauri: Kununua gari isiyoizidi 16m

Ushauri: Kununua gari isiyoizidi 16m

Aeronautical

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2019
Posts
217
Reaction score
396
Habari za jioni ndugu zangu,
Sina uzoefu na magari ila nimejichanga na nimepanga kununua gari isiyozidi 16M na yenye cc isiyozidi 1490cc mpaka 1990cc. Kwa muonekano wa nje mana sio mzoefu wa magari nimevutiwa na Toyota Runx, Allex na Premio ( Mawazo yanaweza kubadilika kulingana na ushauri wenu). Naomba ushauri wenu kwa kuzingatia gharama za maintenance na ulaji wa mafuta. Ahsanteni.
 
TUKUULIZE KWANZA UNATEGEMEA NINI KWENYE HIYO GARI?

unaangalia vigezo gani muhimu kabla...

maana siku hizi magari mengi
 
Kabla ya kununua gari, angalia hizi factors.
1. Buying cost.
2. Fuel cost.
3. Services cost.
4. Mazingira uliyopo.
5. Matumizi uliyokusudia.
6. Interest zako.

Kwa maelezo yako, gari zinazokuhusu.
-Runx
-Allex
-Premio
-IST
-Spacio

Kwa ushauri wangu ningekushauri kuchukua Spacio (New model)kwa pesa hiyo na huenda chenji ikabakia, kwa kuwa ina space nzuri ndani, iko comfortable, ina trend, imara kimtindo na ina heshimika (gari ya kifamilia, sio kihuni fulani)
 
Kama mara yako ya kwanza kununua gari chukua gari ya taifa IST usichukue ya cc 1200 chukua ya 1400 na ushee na kama ni mtu wa safari chukua ya kuanzia mwaka 2008 ya cc 1700 na ushee
 
Kama mara yako ya kwanza kununua gari chukua gari ya taifa IST usichukue ya cc 1200 chukua ya 1400 na ushee na kama ni mtu wa safari chukua ya kuanzia mwaka 2008 ya cc 1700 na ushee
Hahahaha mi naona RunX ndio imekaa kinyamwezi sana hata ukiitia 17" rims inasimamia ukucha kweli
 
Back
Top Bottom