Wala usijisumbue sana, Labda kama wewe ni Dr au Unandugu yako mwenye taaluma ya udaktari.Anayeweza ku establish kuwa daktari ni mzembe ni watu wenye taaluma hiyo Na nafahamu pia wanalindana sana.Unaweza ukapewa lundo la misamiati ya kitabibu juu ya kifo cha mgonjwa ambayo hutakaa uelewe.Kwa nchi masikini kama TZ kumshitaki daktari unaitaji kuwa na knguvu au influence kubwa sana.Wanalindanaga hao.Kuna ndugu yangu mtito wake alipata ulemavu wa mkono kwa uzembe wa nesi ambao wenzake walikiri.ndugu wakafatilia wakachemsha.
du! mkuu yaani nisijisumbue? niridhike tu na makosa yao? sasa lini hali iabadilika watu wasipokumbushwa uwajibikaji?
mkuu hapo umechemsha,..we unajua kazi ya morphine? indications zake? contraindications? morphine ni pain killer tu bro..siyo tiba ya ugonjwa wowote..na kwasababu mgonjwa wako anaumwa sana na unampenda.. haimaanishi lazima apewe morphine! morphine ni kama ile heroine mateja wanayojidunga..siyo tiba..ni kisindikizio ukiwa unakaribia kufa au una maumivu makali sana..pole sana kama ulikuwa unahisi angepona labda kama angepewa morphine..pole sana