Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Watu muhimu katika maisha yako ni wale ambao wameamua kushea maisha na wewe hivyo uwajali sana
Unaweza kuishi maisha marefu au mafupi,ila jali sana ujana wako
Vitu ni vitu tu,usiwekeze sana sana katika vitu ila katika mda na uzoefu
Wivu unaharibu mahusiano,jifunze kumwamini mwenzako,je ni nani mwingine unapaswa kumuamini?
Watu siku zote wanasema hakikisha unafanya kazi unayoipenda,ila hilo sio wazo au ushauri mzuri,kazi nzuri ni ile ambayo unaweza kuipenda baadhi ya siku,kuivumilia baadhi ya siku na ukakidhi mahitaji yako,kwani hakuna mtu ambaye anaipenda kazi yake kila siku.
Usichukulie maisha kwa umakini sana hata pale mambo yanapokuwa magumu na hayaeleweki,jaribu kucheka kwani maisha ndivyo yalivyo
Watoto wanakuwa haraka sana,kwahiyo hakikisha unakuwa na mda wa kufurahi nao
Usichukue mawazo ya mtu kama Ufunuo,unaweza kuomba ushauri kwa mtu mnaye heshimiana halafu linganisha na mazingira yako kisha fanya uamuzi
Lipa madeni yako na uwe huru
Unapokuwa na ndoto ya kufanya jambo gumu wewe jaribu kufanya tu
Unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza,jua kwamba hujui kuhusu yeye,unachoona mbele yako ni jinsia yake,mavazi yake na mwonekano wake.
Ijumaa Mubarak
Ni hayo tu!