Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Balozi Malamula hivi karibuni ametoa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!

Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.

1622882967318.png


Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​



Freedom is coming tomorrow!!!!!!!!!!!!!!!


Malamula atoa kauli kuhusu uraia pacha!!!!!!!


Mweleko mpya kwa uraia pacha

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz



Mweleko mpya kwa uraia pacha​


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali inalifanyia kazi suala la uraia pacha na kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Pia, alisema wizara yake iko tayari kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) kupiga kura endapo watapata ridhaa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa sababu ni rahisi kwa kutumia teknolojia.

Balozi Mulamula alisema hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili alipotembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imetambua suala la uraia pacha linakwenda sambamba na ushiriki wa diaspora; na watu wengi, wakiwamo wabunge wamekuwa wakionyesha utayari wao.

“Tukiwa bungeni kuna mbunge mmoja aliondoa shilingi mpaka tumpe majibu, wakati ule zamani tukienda bungeni walikuwa wanasema ‘bwana wee usituambie habari za diaspora, wanakula kuku kwa mrija, wachague wanataka wapi, huwezi kupata huku ukapata kule’. Sasa mtazamo umebadilika, wao ndio wanaotaka,” alisema Balozi Mulamula.

“Wabunge wengi wametoka diaspora, nikawaambia kama mnalitaka hili basi, na ninyi ni watunga sheria, sisi tunalifanyia mkakati wa kisera, lakini likija kwenye sheria ninyi wabunge ndiyo mtusaidie tuipitishe.”

Balozi Mulamula alisema tangu akiwa balozi, msisitizo wake ni kwamba huwezi kumwondolea mtu haki ya kuzaliwa katika nchi aliyozaliwa.

Alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wamekwenda kutafuta maisha na wako kwenye fani tofauti, ukiwamo udaktari na biashara, hivyo, wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

“Ningekuwa na uwezo ningelimaliza hata jana, ingekuwa imenipa amani sana, hasa kukuza ushiriki wa diaspora. Mtazamo umebadilika, si kama huko nyuma, kwa hiyo mimi naamini kabla ya mwisho wa mwaka huu, tutakuwa tumelipatia suluhu hili la uraia pacha,” alisema.

Alisema suala la uraia pacha lilitakiwa lipite katika mchakato wa mabadiliko ya katiba, lakini ilionekana si suala la kuingia kwenye katiba, bali kuliwekea sheria maalumu kama zilivyofanya Ethiopia na India.

“Kubadilisha Katiba ni mlolongo mrefu, lakini ikishaingia kwenye katiba halafu ukaja utawala mwingine hauitaki, unaitoaje? Kwa hiyo kukiwa na sheria inawalinda zaidi.

“Sasa tumesema tunavyoainisha hii sera yetu ya mambo ya nje, tuko kwenye mkakati wa kuweza kuja na programu maalumu wanayoita hati maalumu zinazowatambulisha Watanzania walioko nje,” alisema Balozi Mulamula.

Suala la uraia pacha ni miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na wananchi wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC) inakusanya maoni ambayo yaliwekwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba kisha kupitishwa kwenye Katiba inayopendekezwa.

Ibara ya 72 ya Katiba Pendekezwa inasema: “Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi maalumu kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.”

Wadau wazungumza

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema nchi zilizoruhusu uraia pacha duniani kote zimepiga hatua kiuchumi kwa sababu zimewajengea diaspora kujiamini na kupata haki kama raia wa nchi zao.

Mbatia alitolea mfano Kenya akisema mwaka jana fedha zilizotoka kwa diaspora kwenda Kenya zilikuwa ni Dola 4.4 bilioni za Marekani ukilinganisha na Dola 380 milioni ambazo diaspora walirudisha hapa Tanzania.

“Ili kujenga confidence ya diaspora, uraia pacha ni muhimu. Kutojiamini ndiyo sababu ya kuwekea vikwazo suala hili, tuangalie mizania ya kiuchumi zaidi ili tufanye maamuzi sahihi,” alisema Mbatia.

Diaspora kupiga kura

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
 
Naunga mkono HOJA.

Hofu ya wapingaji ni kuwa nchi ikiruhusu uraia pacha, wataochukua uraia huko kwingine wanaeza kuwa Wazalendo zaidi huko jambo ambalo si kweli.

Mchina akija Tanzania akanunua uraia, hawezi kuipenda Tz kuliko huko alikozaliwa.

Damu ni nzito kuliko maji, wahenga walisema..
Ni makosa kulingalisha uraia wa kuzaliwa na ule wa kununua ili upate maslahi fulani.

Ni vizuri Uraia pacha uruhusiwe wananchi wawe huru kupata fursa nyingi huko nje
 
Naunga mkono HOJA..

Hofu ya wapingaji ni kuwa nchi ikiruhusu uraia pacha, wataochukua uraia huko kwingine wanaeza kuwa Wazalendo zaidi huko jambo ambalo si kweli.

Mchina akija Tz akanunua uraia, hawezi kuipenda Tz kuliko huko alikozaliwa.

Damu ni nzito kuliko maji, wahenga walisema..
Ni makosa kulingalisha uraia wa kuzaliwa na ule wa kununua ili upate maslahi fulani.

Ni vzr Uraia pacha uruhusiwe wananchi wawe huru kupata fursa nyingi huko nje
Sawa Mkuu, ila angalia kwamba uraia pacha mara nyingu haununuliwi. Inawezekana kwamba kuna nchi ikiwa utakuwa na mtaji mkubwa wa kuwekeza, basi unapewa uraia pia. Lakini tusitafsiri kwamba watu wa nje watakuja Tanzania kununua uraia wa Tanzania.

Ndio maana nikasema, tunaporuhusu uraia pacha, tuna uhuru wa kuweka kanuni zetu. Na tuna uhuru wa kuamua ikiwa mtu anaeleta mtaji wa kiasi fulani cha fedha anastahili kupewa uraia au la. Tunaweza kusema apewe permanent residence badala ya uraia, ambao tutampa baada ya miaka labda mitano ya kuishi nchini.
 
Mleta mada, hoja iwe moja:- Uraia pacha tu, faida na hasara zake. Usichanganye na mengine itakutoa kwenye mstari.

Mawazo ya kizamani. Wanasema Tanzania inahitaji ajira, wawekezaji, wakati kuna watanzania kwa mamilioni wanaishi nje.

Mitaji yao, know how, elimu, exposure ingeweza kusaidia Taifa kwenye nyanja nyingi.
 
Wakati watoto wao wana uraia pachaa wameandaliwa kisiasa watawale sasa wanashindwa kuwaandaa kiuwezaji (invester) ndio maana wanaona wivu kwa wenzao watoto wa maskini walienda kwa harakati zao binafsi kwamba watatoboa zaidi yao na kufungua macho raia
 
Nchi pekee zilizobaki Afrika kuruhusu uraia pacha ni
  • Tanzania
  • Equatorial Guinea
  • DRC
  • Lesotho
  • Malawi
  • Zambia
  • Cameroon (nadhani hawa wameruhusu sasa)
  • Ethiopia (nadhani wameruhusu sasa)
  • Liberia (Sielwi ilikuwaje walikuwa na raisi mwenye uraia wa wa nchi nyingine, Ellen Johnson Sirleaf)
  • Eritrea
Sasa kama huu sio udungaembe ni nini?
 
Tunawaonea wivu nyinyi diaspora ?

Kwa hiyo diaspora mko vizuri kuliko sisi ?

Sasa kwa nini tuhangaike kubadilisha sheria kuwasapoti watu ambao wanasema tayari wako njema na wanatukashfu tuliopo hapa nchini?

Hoja nyepesi za wana diaspora ndio hizi maskini ya Mungu.
Ndio, kama sababu zenu ni zile za Mbwa mwitu kumwambia mwanakondoo aliyezaliwa mwaka huu kwamba wewe mwaka jana ulinitukana, kama sio wivu unawasumbua ni kitu gani? La sivyo sababu zenu za uzalendo na usalama ni za kitoto sana. Angalia hiyo ramani hapo juu. Tutakuwa madungaembe hadi lini?

Kwa taarifa yako mie sio Diaspora lakini naona umuhimu wa uraia pacha.
 
Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
 
Yaani kuna watu wana roho mbaya na wivi zaidi ya shetani ibilisi. Hawapendi kabisa kuona mtu mwingine anafanikiwa hasa ikiwa yeye hatakaa apate hiyo nafasi. Watu wana kitabia cha ovyo sana cha "wote tukose"
Ndio maana hii nchi haiendelei, Roho mbaya na wivu ni laana Kubwa sana, ukiwaangalia usoni, ukiwasikiliza ni umasikini mtupu umejaa
 
Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
Mkuu nimesema angalia hiyo ramani ya nchi za Afika zilizoruhusu uraia pacha, halafu ukiwa na hoja za msingi uraia pacha wao umewauaje njoo tuongee.

Na nimesema uraia pacha hauji automatically. lazima uombe. Kama mtu wa nje anaomba kuwa raia pacha na Tanzania na tuna sababu za msingi za kumkatalia, basi tutamkatalia.
 
Wakati watoto wao wana uraia pachaa wameandaliwa ki siasa watawale sasa wanashindwa kuwaandaa kiuwezaji (invester) ndo mana wanaona wivu kwa wenzao watoto wa maskini walienda kwa harakati zao binafsi kwamba watatoboa zaidi yao na kufungua macho raia
Point nzuri, ila watoto wao hawana uraia pacha Mkuu, labda kwa siri. Maana Tanzania bado hairuhusu.
 
Back
Top Bottom