Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi

Hoja yako kuhusu Wahindi inaonekana msingi wake ni Uhamiaji hawako makini, wanachukua rushwa kutoa vibali.

Hapo ni kuimarisha hii idara iwe na watu makini. Diaspora wengi ni watu weusi kama wewe. Wahindi wanaweza kuwa less than 5%.
 
Ningewashauri wale wote wanaoona faida za Tanzania kuwa na uraia pacha watoe msisitizo wao kwenye hii thread
Faida zipo kubwa sn nakupa mfano mmoja tu ambao utawafunua watu katik kipindi cha mwaka wa 2019/20.

Remittance flows to Sub-Sahara African countries ilikuwa kiasi cha over $50 BILLION DOLLARS sasa hebu tizama hicho kiasi cha pesa .
 
Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.

Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
 
Ndio maana nasema CCM siku zote inapenda kutumia ujinga wa Watanzania kama mtaji...

Hoja wanazotoa ni nyepesi sana na zisizo na mantiki ! Mara utasikia matishio ya kiusalama mara uzalendo unashuka! Na yote haya hayathibitishwi bali ni hadithi tu kutoka kwa viongozi waongo waongo..

Kwa mwaka wa 19 tangu nimetoka nyumbani nimeona tofauti kubwa sana hasa kimaendeleo na kimtazamo , huku nimekutana na watu na kupata marafiki wengi tu hata wa Africa ambazo nchi zao zinaruhusu dual citizenship sasa najiuliza CCM walishawahi kuchukua maoni kutoka hizo nchi na hawa watu wanachangia mapato kiasi gani kwenye "nchi mama" walizotoka..??

Jibu ni kua hawajafanya tafiti ndio maana hadi leo vijana wengi wa kitanzania wanakosa fursa adhimu mbali mbali kutokana na huduma baadhi za PayPal kutoruhusiwa ila ukiwauliza viongozi hawana majibu

Kiukweli faida zipo ni nyingi ,hali kadhalika hasara zipo japo hazishindi faida ila kiukweli kwa hili "bunge la jiwe" sitarajii kama wataijadili hii hoja na hata siku moja achilia mbali kupitishwa
 
Faida zipo kubwa sn nakupa mfano mmoja tu ambao utawafunua watu katik kipindi cha mwaka wa 2019/20.

Remittance flows to Sub-Sahara African countries ilikuwa kiasi cha over $50 BILLION DOLLARS sasa hebu tizama hicho kiasi cha pesa .

Ukiangalia faida zingine kama direct investment, kuongeza biashara kati ya nchi hizo mbili, transfer of knowledge, ubunifu, investment in elimu, kilimo, afya, utalii, technology.

Pia work ethics and their self confidence will rub off others. (Wanafanya kazi kwa bidii na kujiamini itasaidia wengine. Sababu USA na EU Lazima ufanye kazi kwa bidii, ujiamini,uthubutu, uwe vizuri zaidi ya wazungu wengi, mvumilivu na uwezo kusoma vitu, mazingira haraka. Otherwise hutoboi.
 
Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.

Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.

Ni hivi kuna advantages kuwa na uraia wa nchi hizo, baadhi ni urahisi wa kusafiri rahisi kupata kazi, matibabu bure, kusoma (bure nchi zingine au mikopo nafuu), kufikia ngazi za juu Serikalini, hata sekta binafsi. Wanakuona ni mwenzio.

Wengine wamezaliwa huko, wazazi wao walipokuwa wanasoma, katika harakati za kupambana na maisha.

Kuna benefits flani unapata ukiwa Raia, wasio Raia wanaweza wasipate. Hata Tanzania unaweza kuona tofauti iliyopo kati ya Raia na wasio Raia.
 
Issue ni ile ile tu mtauwa uzalendo

Uzalendo ni kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yako kwa sababu za utamaduni, historia.

Diaspora wengi wanasaidia sana ndugu zao, jamii, Taifa Serikali inapata hard foreign currency zinazotumika kununua mahitaji muhimu. Pia wengi wanatoa michango kujenga shule, hospitali, kusomesha wanafunzi etc.

Nchi za Kaskazini na Magharibi ya Afrika siku zote wanachukua kombe la Afrika. Pia Club zao zinafanya vizuri sana.

Ukiangalia wachezaji wao kama Algeria, Nigeria, Ghana, Morocco, Tunisia, Ivory Coast, Cameroon hata Shelisheli wachezaji wao wengi wanacheza ulaya, wengi wamezaliwa Ulaya. Wakicheza mpira wanacheza kwa nguvu kuliko wazalendo wa Tanzania.

Wanacheza kwa uzalendo wa hali ya juu, ukijumlisha na technical superiority, exposure, self confidence unapata decent team.
 
Diaspora wa kitanzania aliopo Nje kama ana nia kweli ya kuwekeza hapa Tanzania sidhani swala la uraia pacha ni kikwazo.
 
Marekani ni tajiri na inadumu na hali nzuri kwa sababu ya mchanganyiko wa watu, kuna wahindi, wachina, waarabu mpaka wamasai wapo kule.

South Africa ni nchi yenye uchumi mkubwa kwa sababu ya mchanganyiko mkubwa wa watu wa rangi mbalimbali wanaoishi pamoja.

Watanzania wenzetu ambao wapo nje wanao mchango mkubwa sana wa kuipeleka Tanzania mbali kiuchumi, wanao uzoefu (exposure) wa hali ya juu kwenye masuala mengi. Sisi wenyewe kwa kubagua wenzetu hatuwezi kufika mbali.
 
Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
Ni mhindi gani wa kuhangaika na ajira za kulipwa milioni kwa mwezi? Labda mhindi koko
 
Ndio maana nasema CCM siku zote inapenda kutumia ujinga wa Watanzania kama mtaji...

Hoja wanazotoa ni nyepesi sana na zisizo na mantiki ! Mara utasikia matishio ya kiusalama mara uzalendo unashuka! Na yote haya hayathibitishwi bali ni hadithi tu kutoka kwa viongozi waongo waongo..

Kwa mwaka wa 19 tangu nimetoka nyumbani nimeona tofauti kubwa sana hasa kimaendeleo na kimtazamo , huku nimekutana na watu na kupata marafiki wengi tu hata wa Africa ambazo nchi zao zinaruhu dual citizenship sasa najiuliza CCM walishawahi kuchukua maoni kutoka hizo nchi n hawa watu wanachangia mapato kiasi gani kwenye "nchi mama" walizotoka..??

Jibu ni kua hawajafanya tafiti ndio maana hadi leo vijana wengi wa kitanzania wanakosa fura adhimu mbali mbali kutokana na huduma baadhi za PayPal kutoruhusiwa ila ukiwauliza viongozi hawana majibu

Kiukweli faida zipo ni nyingi ,hali kadhalika hasara zipo japo hazishindi faida ila kiukweli kwa hili "bunge la jiwe" sitarajii kama wataijadili hii hoja na hata siku moja achilia mbali kupitishwa
Makando kando ya ujamaa bado yanatuathiri na ukiongezea wanasiasa kulipwa mishahara minono wao na watoto wao wanaishi maisha mazuri kwa hyo izo kelele za diaspora wala haziwasumbui
 
Diaspora wa kitanzania aliopo Nje kama ana nia kweli ya kuwekeza hapa Tanzania sidhani swala la uraia pacha ni kikwazo.

..anaweza kuwekeza kwa kuwatumia wazazi au ndugu zake.

..sokomoko linakuja kukitokea bahati mbaya kuwa aliyeandikishwa mali amefariki.

..au aliyeandikishwa mali amekosa uaminifu huyu diaspora anakuwa hana namna ya kupata haki yake.
 
Back
Top Bottom