Trubetzkoy
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 380
- 747
Salama humu ndani?
Ushauri wa bure kwa ndugu zangu wa people's power. Ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa mambo yanayokwamisha vuguvugu na harakati za kupigania mageuzi nchini ni kwamba watanzania walio wengi hawajitambui na hata wale wachache wanaojitambua bado hawatambui haki na wajibu wao katika taifa.
Ni ngumu sana kumwambia mtu adai haki ilihali haki hiyo haijui, pia ni ngumu kumwambia mtu asimame katika nafasi yake ilihali hajui nafasi yake ni ipi katika jamii. Mtu asiyetambua nafasi, haki na wajibu wake ni ngumu sana kumuelewesha akakuelewa.
Ushauri!
Kwakuwa ndani ya Chadema kumesheheni wanasheria nguli kama Kibatala, Mahinyila na wengine wengi ni vema sasa Chadema waanzishe shule ya katiba na sheria kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye majukwaa ya wazi lengo likiwa ni kutoa elimu ya utambuzi wa masuala ya kisheria.
Tuliona wakati Hamphrey Polepole alipoanzisha shule ya siasa ilichukua muda mfupi tu kujizolea maelfu ya watanzania wafuasi waliokuwa wakimsikiliza na ukweli ni kwamba sessions zake zilitokea kupendwa sana ndani ya kipindi kifupi tu.
Kwakuwa kuiga yaliyo mema si ujinga wala fedheha Chadema tumieni shule ya siasa ya ndugu Polepole kama skeleton. Mnaweza kuandaa sessions hata moja kwa siku maalumu katika kila wiki na wanasheria wenu wakagawana hizo sessions, let's say wiki hii tunapata shule kutoka kwa Peter Kibatala next week tunapata shule kutoka kwa Peter Madeleka uone mambo yatakavyonyooka.
Jikiteni kwenye kutoa elimu ya utambuzi huku kwa ground wanaojitambua ni wachache na hao wachache ni wachache wanaotambua haki na wajibu wao!