Pre GE2025 Ushauri kwa CHADEMA ili kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Jinsi ya CHADEMA kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa 2025.

1. Kwanza, mgombea urais wa CHADEMA apatikane kwa njia ya primaries. Hii ndio njia tuliyokuwa tunaitumia huko nyuma. Hata wakati Mbowe anagombea urais wa 2005, tulitumia mfumo wa primaries. Kwa maana nyingine wanachama ndani ya Kanda ndio wanaopiga kura kumchagua mgombea urais na baadaye kuthibitishwa na Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama. Chama kinaweza kufanya primaries kwa mfumo wa Kanda au mikoa. kura wapige wanachama wa CHADEMA sio Viongozi pekee.

Hizi primaries zitaweka uwazi wa wagombea urais kwa wananchi wawatambue. Maana primaries zinatakiwa kuanza mapema sana Kama mwezi wa kwanza 2025. kila Kanda itakuwa na muda wake wa kampeni na uchaguzi. Hivyo primaries zinaweza kuchukua hata miezi sita kuisha.

Faida ya primaries.

I. Inaruhusu uwazi
II. Ina ruhusu coverage Kwenye media.
III. Inaruhusu wanachama kujua sera za wagombea kwa uwazi.
IV. Inaruhusu midahalo baina ya wagombea urais ndani ya chama.

2. Pili, CHADEMA ije na slogan ya kampeni ambayo itaweza kuwafikia wananchi bila tatizo na kueleweka. kwa maana nyingine CHADEMA wabuni slogan ambayo inaendana na uhalisia wa hali ya wananchi kwa Sasa. kwa mfano ningependekeza CHADEMA waje na slogan inayosema Mkataba na wananchi. Hii maana yake ni kwamba CHADEMA itabainisha mambo kumi ambayo itayafanyia kazi kwenye miaka mitano na kutengeneza kwenye mfumo wa mkataba. Ambapo kila eneo watakalokuwa wanafanya kampeni za ugombea urais watakuwa wanasign huo mkataba na wananchi wakimaliza mkutano. Pia huo mkataba wagawiwe wananchi wausome bila kujali chama gani. Wananchi wengi wakiusoma huo mkataba na kuuelewa CHADEMA watakuwa wamefanikisha agenda yao kwa wananchi na hivyo kupata wapiga kura wapya na kuwabakiza wapiga kura wazamani.

Faida za Slogan ya Mkataba na wananchi
I. Hii itaonesha CHADEMA ipo tayari kufanya kazi na wananchi na kuwatumikia.
II. Hii itafafanua kwa ufupi Sana yote ambayo CHADEMA inalenga kuyafanya.
III. Hii itajenga uwajibikaji kwa wananchi .

3. Tatu, CHADEMA ijikite kwenye kupata kura za vijana na wa wanawake. Hili ndio kundi kubwa la wapiga kura. Bila kupata uungwaji mkono wa vijana au wanawake ni kazi Sana kushinda uchaguzi wa urais. Njia moja wapo ya kuwapata vijana na wanawake ni kuwapa nafasi za kugombea majimboni . Na pia kujikita kwenye agenda ya Ajira na uwezeshwaji na kuifafanua vizuri. Kwamba serikali ya CHADEMA itaongeza fursa nyingi za ajira kwa vijana na kuwasaidia kwenye maeneo ya ubunifu na pia kuwawezesha wanawake kwenye program ya ujasiriamali. Hii itajenga uwaminifu na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wanawake kwenda na hata vijana pia.

4. Nne, CHADEMA ijikite Sana kwenye agenda ya uchumi. Namna gani itapunguza Deni la nje na la ndani. Namna gani itapunguza mfumuko wa bei, namna gani itakuza Ajira, namna gani itaweka ruzuku kwenye simenti, nondo namna gani itakufanya Kodi na kuongeza mapato , namna gani itapambana na ufisadi. kwa mfano suala la ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ni kuwasaidia wananchi ili wajenge nyumba kwa unafuu kuliko Sasa gharama zipo juu. Pia CHADEMA waelezee namna gani watakuza sekta ya usafiri ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Ni vizuri Sana kampeni za CHADEMA 2025 zijikite huko kwenye uchumi na sio vijembe na malalamiko. CHADEMA ipeleke ujumbe wa uchumi bora kwa wananchi na kuifafanua vizuri namna gani ya kufufua huo uchumi. Ili kufanikisha hili, CHADEMA baada ya kumpata mgombea wao wa Urais inabidi waunde kamati ya wataalamu wa uchumi ambao wataelezea na kuifafanua agenda ya uchumi kwa wananchi wakati wa kampeni.

5. Tano, CHADEMA ijikite kwenye katiba Mpya. Hasa kwenye mambo ya Usalama na ufisadi. Leo mtu anatekwa lakini hakuna anayewajibika au mtu anashutumiwa kwa ufisadi ila hawajibishwi. So ajenda ya Katiba Mpya isiwe kwenye vyeo au Muungano tu bali mambo mengine Kama Usalama, ufisadi, mfumo wa kiuchumi kwa sasa hauleweki maana katiba inasema ujamaa ila ukija kwenye uhalisia sio ujamaa ni mixed grill economy, ceiling ya kukopa nje, kuthibitisha nafasi za uteuzi, kuondoa wakuu wa mikoa na Wilaya . Kwenye hili la Katiba mpyana CHADEMA ijitoe kwenye mtego wa kuonekana inataka Katiba Mpya kisa madaraka bali ijikite kwenye reforms zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nitaongeza mengine baadae kwa sasa haya yanatosha. Long live CHADEMA.

From Econonist
 
Tunayafanyia kazi tuchukue ya msingi au yote ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…