Uchaguzi 2020 Ushauri kwa CHADEMA kuelekea Oktoba 2020

Chivundu

Platinum Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
7,781
Reaction score
6,966
Wanabodi.
Nawashauri Chadema kwamba:

Andaeni ajenda msiandae wagombea. Wagombea wakipatikana kupitia michakato mliojiwekea watembee katika ajenda zenu kuu kulingana na jinsi nchi ilivyo kwa sasa. Msifanye wagombea kua ajenda hamta pata kura.

Hamuwezi kupata kura nyingi katika mazingira ya huruma "public sympathy" kama ambavyo sasa inaonekana bila ajenda zitakazotokana na mapungufu ya selikali ya sasa.

Ile dhana inayozidi kujengeka kwamba kura zitapatikana kwa kuwa "Mgombea" alipigwa risasi na alifanyiwa hila italeta siasa lakini haitaleta kura kwa kizazi cha sasa ambacho "unemployment rate" ni kubwa mno.
Andaeni na kuanza kuziuza ajenda zenu mbadala za nchi. Ajenda hizo ndizo zitazaa Ilani "manifesto".

Mtakumbuka aenda ya ufisadi ndiyo iliwapa umaarufu. Ufisadi na rushwa kubwa kubwa bado zipo,sijajua kwanini mliachana na hii ajenda. Jitahidi kuelekea kampeni kuja na programu ya kupata mawazo ya wananchi kupitia platforms mbalimbali nchi nzima ili mpate ajenda itakayo zaa ilani nzuri yenye kugusa makundi yote na iitwe ilani ya wananchi sio ya chama ili mgombea wenu aje aiuze kwa wananchi.

Chama chenye wanachama,madiwani na wabunge nchi nzima kinaweza kuandaa programu ya kupata mawazo ya wananchi,mawazo yakachambuliwa ikapatikana ilani nzuri yenye ajenda za kugusa maisha ya wananchi.

Hii ni kwa vyama vyote: vyama viondokane na ile "dhana" ya watu flani "wasomi" kuweka mawazo yao katika karatasi na kuyaita "ilani" au "manifesto" na kuja kuiuza kwa wananchi.

Ilani angalau itokane na mawazo ya wananchi hata kwa asilimia 80% ndipo mtapata uungwaji mkono. Fikiria ishu ya ukosefu wa ajira kwa sasa ni ishu kubwa sana kuliko inavyofikiriwa au kuchukuliwa na watawala.

Kuwaacha wagombea kuwa ajenda kutaleta siasa lakini hakuwezi kuleta kura na uungwaji mkono mkubwa. Itikadi,falsafa,ajenda na sera ndio moyo wa siasa za chama chochote.

Nawasilisha.
 
Jitahidi kuelekea kampeni kuja na programu ya kupata mawazo ya wananchi kupitia platforms mbalimbali nchi nzima ili mpate ajenda itakayo zaa ilani nzuri yenye kugusa makundi yote na iitwe ilani ya wananchi sio ya chama ili mgombea wenu aje aiuze kwa wananchi.
LOoo, mkuu 'aloycious',

Unawakumbusha shuka wakati kumekucha tayari?

Wakati huu ndio wawaendee wananchi kwa kazi waliyotakiwa kuifanya kwa uendelevu miaka mitano iliyopita?.

Ninakubaliana na baadhi ya uliyowashauri, lakini hata wewe mwenyewe umechelewa kutoa ushauri waufanyie kazi kungali mapema.

Nadhani kuna sababu wasizotaka kuzieleza CHADEMA kuhusu sera zao, maanake ni nadra sana kusikia viongozi wakizungumzia mambo yanayosimamiwa na chama chao ili wananchi wayaelewe.

Haya mambo siyo ya kusubiri kuyaelezea wakati wa kampeni peke yake. Wakati wa kampeni ni kutoa ufafanuzi sehemu zinazohitaji kufafanuliwa, au zinazopindishwa na wapinzani wao.

Safari hii Magufuli katika miaka yake mitano hii amekwishawatengenezea ajenda nzito mno za kuwapelekea wananchi.

Wakishindwa kuzieleza kwa wananchi wajilaumu tu wao wenyewe kwa kukosa uwezo wa kuzijengea hoja.

Kwa mfano: Ni mwananchi gani asiyeweza kusimama na kusikiliza maelezo ya umhimu wa utawala bora kwa nchi yetu!

Ni mwananchi yupi asiyependa haki zake zilindwe, kama haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi anaotaka yeye bila ya kuwa na shaka ya kura yake kuharibiwa au kutohesabiwa kabisa.

Ni mwananchi gani asiyetaka kupata na kutoa habari bila ya hofu ya kudhaniwa kuwa anavunja sheria.

Ni mwananchi gani asiyependa kuona wawakilishi wake bungeni wakifanya kazi kwa niaba yake bila ya kuingiliwa na/au kufichwa kinachotakiwa kuonekana kinafanyika wakati akifanya kazi hiyo.

Umoja wetu wa kitaifa na mshikamano wetu haujawahi kutetereka kama ulivyofikia wakati wa miaka hii mitano. Wewe unadhani wapinzani wakilieleza hili kwa wananchi, bado wananchi watakuwa hawaelewi kitu?

Ajenda kazitengeneza nyingi mno Magufuli, kiasi kwamba itawawia vigumu wapinzani wachague zipi za kuwaeleza wananchi katika muda mfupi wa kampeni.
 
Nliwaambia mapema Waache hiyo tabia hawakusikia kila mtu apambane na Hali yake
Karibuni Norway tule maisha hapa
 
Chadema imekwisha fanya kila kitu , hii ndio kazi kubwa iliyofanywa na ofisi ya Katibu Mkuu
 
Yupi.

Mashinji?

Kama angekuwa na ari ya kufanya kazi mhimu kama hii ndani ya CHADEMA kweli angefikiria hata kuhama chama?

Hapa unanilisha matango pori tena mchana mzima rafiki yangu Erythro.

Najua Mnyika anaweza kuifanya kazi hiyo, tena kwa ufanisi sana, lakini si kaingia juzi tu? Au yeye aliianza akiwa naibu nyuma ya mgongo wa katibu mwenyewe?
 
uchaguzi mkuu wa Chadema ulifanyika desemba 2019 , kwa siasa za Tanzania hii si juzi
 
Yupi.

Mashinji?

Kama angekuwa na ari ya kufanya kazi mhimu kama hii ndani ya CHADEMA kweli angefikiria hata kuhama chama?

Hapa unanilisha matango pori tena mchana mzima rafiki yangu Erythro.

Najua Mnyika anaweza kuifanya kazi hiyo, tena kwa ufanisi sana, lakini si kaingia juzi tu? Au yeye aliianza akiwa naibu nyuma ya mgongo wa katibu mwenyewe?

Tatizo uwanja wa siasa haupo sawa Kati ya CCM na wapinzani...

Pqmoja na Hilo CDM wanapaswa kuwa na sera makini za maendeleo na mawazo mbadala...
 
Vyote ulivyoshauri tayari vilishaandaliwa. Sanasubiri filimbi ipigwe kuruhusu kampeni. Tena mwaka huu kuna agenda nyingi sana

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi.
Nawashauri Chadema kwamba:

Andaane ajenda msiandae wagombea. Wagombea wakipatikana kupitia michakato mliojiwekea watembee katika ajenda zenu kuu kulingana na jinsi nchi ilivyo kwa sasa. Msifanye wagombea kua ajenda hamta pata kura.

Hamuwezi kupata kura nyingi katika mazingira ya huruma "public sympathy" kama ambavyo sasa inaonekana bila ajenda zitakazotokana na mapungufu ya selikali ya sasa. Ile dhana inayozidi kujengeka kwamba kura zitapatikana kwa kuwa "Mgombea" alipigwa risasi na alifanyiwa hila italeta siasa lakini haitaleta kura kwa kizazi cha sasa ambacho "unemployment rate" ni kubwa mno.
Andaeni na kuanza kuziuza ajenda zenu mbadala za nchi. Ajenda hizo ndizo zitazaa Ilani "manifesto".

Mtakumbuka aenda ya ufisadi ndiyo iliwapa umaarufu. Ufisadi na rushwa kubwa kubwa bado zipo,sijajua kwanini mliachana na hii ajenda. Jitahidi kuelekea kampeni kuja na programu ya kupata mawazo ya wananchi kupitia platforms mbalimbali nchi nzima ili mpate ajenda itakayo zaa ilani nzuri yenye kugusa makundi yote na iitwe ilani ya wananchi sio ya chama ili mgombea wenu aje aiuze kwa wananchi.

Chama chenye wanachama,madiwani na wabunge nchi nzima kinaweza kuandaa programu ya kupata mawazo ya wananchi,mawazo yakachambuliwa ikapatikana ilani nzuri yenye ajenda za kugusa maisha ya wananchi. Hii ni kwa vyama vyote: vyama viondokane na ile "dhana" ya watu flani "wasomi" kuweka mawazo yao katika karatasi na kuyaita "ilani" au "manifesto" na kuja kuiuza kwa wananchi.

Ilani angalau itokane na mawazo ya wananchi hata kwa asilimia 80% ndipo mtapata uungwaji mkono. Fikiria ishu ya ukosefu wa ajira kwa sasa ni ishu kubwa sana kuliko inavyofikiriwa au kuchukuliwa na watawala.

Kuwaacha wagombea kuwa ajenda kutaleta siasa lakini hakuwezi kuleta kura na uungwaji mkono mkubwa. Itikadi,falsafa,ajenda na sera ndio moyo wa siasa za chama chochote.

Nawasilisha.
Ushauri mzuri, tumejipanga vizuri katika hilo.
 
LOoo, mkuu 'aloycious',

Unawakumbusha shuka wakati kumekucha tayari?

Wakati huu ndio wawaendee wananchi kwa kazi waliyotakiwa kuifanya kwa uendelevu miaka mitano iliyopita?.

Ninakubaliana na baadhi ya uliyowashauri, lakini hata wewe mwenyewe umechelewa kutoa ushauri waufanyie kazi kungali mapema.

Nadhani kuna sababu wasizotaka kuzieleza CHADEMA kuhusu sera zao, maanake ni nadra sana kusikia viongozi wakizungumzia mambo yanayosimamiwa na chama chao ili wananchi wayaelewe.

Haya mambo siyo ya kusubiri kuyaelezea wakati wa kampeni peke yake. Wakati wa kampeni ni kutoa ufafanuzi sehemu zinazohitaji kufafanuliwa, au zinazopindishwa na wapinzani wao.

Safari hii Magufuli katika miaka yake mitano hii amekwishawatengenezea ajenda nzito mno za kuwapelekea wananchi.

Wakishindwa kuzieleza kwa wananchi wajilaumu tu wao wenyewe kwa kukosa uwezo wa kuzijengea hoja.

Kwa mfano: Ni mwananchi gani asiyeweza kusimama na kusikiliza maelezo ya umhimu wa utawala bora kwa nchi yetu!

Ni mwananchi yupi asiyependa haki zake zilindwe, kama haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi anaotaka yeye bila ya kuwa na shaka ya kura yake kuharibiwa au kutohesabiwa kabisa.

Ni mwananchi gani asiyetaka kupata na kutoa habari bila ya hofu ya kudhaniwa kuwa anavunja sheria.

Ni mwananchi gani asiyependa kuona wawakilishi wake bungeni wakifanya kazi kwa niaba yake bila ya kuingiliwa na/au kufichwa kinachotakiwa kuonekana kinafanyika wakati akifanya kazi hiyo.

Umoja wetu wa kitaifa na mshikamano wetu haujawahi kutetereka kama ulivyofikia wakati wa miaka hii mitano. Wewe unadhani wapinzani wakilieleza hili kwa wananchi, bado wananchi watakuwa hawaelewi kitu?

Ajenda kazitengeneza nyingi mno Magufuli, kiasi kwamba itawawia vigumu wapinzani wachague zipi za kuwaeleza wananchi katika muda mfupi wa kampeni.
Hujui kitu mkuu, tumejipanga kuliko mnavyodhania na uzuri ni kuwa kwa dharau na kejeli zenu hamtakuwa na uwezo wa kujibu, kama ni kuchelewa ni nyie mlioamini kuwa kwa kutuzuia kufanya siasa kwa miaka mitano na kununua wale vibaka wachache mkajua Chadema imekufa.Kazi tuliyoifanya kimya kimya miaka hii mitano ndiyo ilipelekea CCM na dola kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 
Ccm inasimamia sera gani??
 
Swadakta
 
Tatizo uwanja wa siasa haupo sawa Kati ya CCM na wapinzani...

Pqmoja na Hilo CDM wanapaswa kuwa na sera makini za maendeleo na mawazo mbadala...
Tatizo la uwanja sawa linafahamika na tulishalisemea sana humu.
Hii leo huhitaji kutegemea majukwaa ya hotuba za mikutanoni kufanya siasa vijijini. Teknoloji ilikwishalisawazisha hilo. Kama CHADEMA hawakufanya siasa vijijini, 'uwanja sawa' kitakuwa ni kisingizio cha wao kutokuwa makini tu.

Walishajua toka mwanzo 'uwanja haupo sawa', kwa hiyo ulitegemea hadi uwanja usawazishwe ndio wafanye siasa? Mbona njia za kufanya siasa zipo nyingi!

Hili la 'sera za CHADEMA' ni shida kubwa. Hazijulikani; lakini hiyo si hoja kwa sasa. Yanayofanywa na utawala uliopo yanatosha kabisa watu kusubiri hizo sera baadae, kazi muhimu ni kuwaondoa hawa wanaotugeuza kuwa mateka wao sasa hivi.
 
Hujui kitu mkuu, tumejipanga kuliko mnavyodhania na uzuri ni kuwa kwa dharau na kejeli zenu hamtakuwa na uwezo wa kujibu, kama ni kuchelewa ni nyie mlioamini kuwa kwa kutuzuia kufanya siasa kwa miaka mitano na kununua wale vibaka wachache mkajua Chadema imekufa.Kazi tuliyoifanya kimya kimya miaka hii mitano ndiyo ilipelekea CCM na dola kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Unanizungumzia mimi wala hunijui. Kosa lako linaanzia hapo.

Mimi nipo huku kijijini, naona yanayofanyika huku huku kijijini kwetu.

Wewe unanilisha upepo tu na majigambo yasiyokuwa namsingi.

Ninachoweza kuwapa mategemeo nacho ni zawadi aliyowapa Magufuli katika miaka yake hii itano. Mkishindwa kuitumia zawadi hiyo ipasavyo mtaanza mipasho mingine, lakini hamkubali kukiri udhaifu wenu.
 
LOoo, mkuu 'aloycious',

Unawakumbusha shuka wakati kumekucha tayari?

Wakati huu ndio wawaendee wananchi kwa kazi waliyotakiwa kuifanya kwa uendelevu miaka mitano iliyopita?.

Ninakubaliana na baadhi ya uliyowashauri, lakini hata wewe mwenyewe umechelewa kutoa ushauri waufanyie kazi kungali mapema.

Nadhani kuna sababu wasizotaka kuzieleza CHADEMA kuhusu sera zao, maanake ni nadra sana kusikia viongozi wakizungumzia mambo yanayosimamiwa na chama chao ili wananchi wayaelewe.

Haya mambo siyo ya kusubiri kuyaelezea wakati wa kampeni peke yake. Wakati wa kampeni ni kutoa ufafanuzi sehemu zinazohitaji kufafanuliwa, au zinazopindishwa na wapinzani wao.

Safari hii Magufuli katika miaka yake mitano hii amekwishawatengenezea ajenda nzito mno za kuwapelekea wananchi.

Wakishindwa kuzieleza kwa wananchi wajilaumu tu wao wenyewe kwa kukosa uwezo wa kuzijengea hoja.

Kwa mfano: Ni mwananchi gani asiyeweza kusimama na kusikiliza maelezo ya umhimu wa utawala bora kwa nchi yetu!

Ni mwananchi yupi asiyependa haki zake zilindwe, kama haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi anaotaka yeye bila ya kuwa na shaka ya kura yake kuharibiwa au kutohesabiwa kabisa.

Ni mwananchi gani asiyetaka kupata na kutoa habari bila ya hofu ya kudhaniwa kuwa anavunja sheria.

Ni mwananchi gani asiyependa kuona wawakilishi wake bungeni wakifanya kazi kwa niaba yake bila ya kuingiliwa na/au kufichwa kinachotakiwa kuonekana kinafanyika wakati akifanya kazi hiyo.

Umoja wetu wa kitaifa na mshikamano wetu haujawahi kutetereka kama ulivyofikia wakati wa miaka hii mitano. Wewe unadhani wapinzani wakilieleza hili kwa wananchi, bado wananchi watakuwa hawaelewi kitu?

Ajenda kazitengeneza nyingi mno Magufuli, kiasi kwamba itawawia vigumu wapinzani wachague zipi za kuwaeleza wananchi katika muda mfupi wa kampeni.

hata mkipewa nchi cdm bado fimbo ya unemployment itawaandama, kutupia lawama serikali kuhusu employment ni uchizi wa akili, swala la mahusiano ya nchi za nje hakuna sehem tumeharibu mahusiano, its easy kama unataka kua na mahusiano mazuri na tz kua na fair playground sasa wewe unataka kila nchi tuwe na mahusiano nayo then mwananchi anaumia bado, kwamba tue na mahusiano mazuri lakini dhahabu ziibiwe? tembo wauliwe? thats a lame excuse, lazima kue na kiongozi mwenye msimamo sio lazima kila sheria iende inavotakiwa lazima zingine zivunjwe mbona china wameshafunga na ofisi za ubalozi wa marekani and vice versa whats hard on that, very lame excuse
 
Unanizungumzia mimi wala hunijui. Kosa lako linaanzia hapo.

Mimi nipo huku kijijini, naona yanayofanyika huku huku kijijini kwetu.

Wewe unanilisha upepo tu na majigambo yasiyokuwa namsingi.

Ninachoweza kuwapa mategemeo nacho ni zawadi aliyowapa Magufuli katika miaka yake hii itano. Mkishindwa kuitumia zawadi hiyo ipasavyo mtaanza mipasho mingine, lakini hamkubali kukiri udhaifu wenu.
Sawa mkuu nimekusoma vizuri.
 
Chadema imekwisha fanya kila kitu , hii ndio kazi kubwa iliyofanywa na ofisi ya Katibu Mkuu

Mkuu hiyo kazi kaifanyia wapi? Hoja ya mleta uzi iko wazi kuwa ajenda ziwe za wananchi, na wala mgombea asiwe ajenda. Mfano mrahisi kwa sasa mwenye nyota ndani ya cdm ni Lisu. Hivyo anatakiwa akisimama aongee matakwa ya wananchi zaidi, na sio matatizo yake. Anatakiwa akimaliza kuongea mahitaji ya wananchi, hayo yakwake aongee kama ziada.

Kwa mvuto alionao Lisu akisimama na kusema kipaombele chake cha kwanza itakuwa ni kutoa ajira kwa vijana, kukuza kilimo na kuboresha masoko, akisema atashusha vifaa vya ujenzi ili kila mtu ajenge nyumba bora, akisema atashusha gharama za matibabu nchini ili kila aweze kutibiwa, huoni hapo atavuta wapiga kura wengi wa ukweli?
 
Wanabodi.
Nawashauri Chadema kwamba:

Andaane ajenda msiandae wagombea. Wagombea wakipatikana kupitia michakato mliojiwekea watembee katika ajenda zenu kuu kulingana na jinsi nchi ilivyo kwa sasa. Msifanye wagombea kua ajenda hamta pata kura.

Hamuwezi kupata kura nyingi katika mazingira ya huruma "public sympathy" kama ambavyo sasa inaonekana bila ajenda zitakazotokana na mapungufu ya selikali ya sasa. Ile dhana inayozidi kujengeka kwamba kura zitapatikana kwa kuwa "Mgombea" alipigwa risasi na alifanyiwa hila italeta siasa lakini haitaleta kura kwa kizazi cha sasa ambacho "unemployment rate" ni kubwa mno.
Andaeni na kuanza kuziuza ajenda zenu mbadala za nchi. Ajenda hizo ndizo zitazaa Ilani "manifesto".

Mtakumbuka aenda ya ufisadi ndiyo iliwapa umaarufu. Ufisadi na rushwa kubwa kubwa bado zipo,sijajua kwanini mliachana na hii ajenda. Jitahidi kuelekea kampeni kuja na programu ya kupata mawazo ya wananchi kupitia platforms mbalimbali nchi nzima ili mpate ajenda itakayo zaa ilani nzuri yenye kugusa makundi yote na iitwe ilani ya wananchi sio ya chama ili mgombea wenu aje aiuze kwa wananchi.

Chama chenye wanachama,madiwani na wabunge nchi nzima kinaweza kuandaa programu ya kupata mawazo ya wananchi,mawazo yakachambuliwa ikapatikana ilani nzuri yenye ajenda za kugusa maisha ya wananchi. Hii ni kwa vyama vyote: vyama viondokane na ile "dhana" ya watu flani "wasomi" kuweka mawazo yao katika karatasi na kuyaita "ilani" au "manifesto" na kuja kuiuza kwa wananchi.

Ilani angalau itokane na mawazo ya wananchi hata kwa asilimia 80% ndipo mtapata uungwaji mkono. Fikiria ishu ya ukosefu wa ajira kwa sasa ni ishu kubwa sana kuliko inavyofikiriwa au kuchukuliwa na watawala.

Kuwaacha wagombea kuwa ajenda kutaleta siasa lakini hakuwezi kuleta kura na uungwaji mkono mkubwa. Itikadi,falsafa,ajenda na sera ndio moyo wa siasa za chama chochote.

Nawasilisha.
Bahati mbaya hawatakubali ushauri wako kwa sababu hawana nia ya dhati wala uzalendo juu ya Taifa letu, you CHADEMA want to imezaliwa kwenye upinzani tu bahati mbaya mzee mtei alisaliti mnakubaliano na waasisi wenzie tofauti kabisa na CCM
 
Back
Top Bottom