Ushauri kwa CHADEMA

Kaniki1974

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2008
Posts
352
Reaction score
22
Nawashauri CHADEMA kuhakikisha hawaibiwi kura huko Busanda kwani wizi wa kura ndio njia pekee iliyobaki kwa CCM sasa kupora ushindi Busanda. Hivyo CHADEMA please msifanye uzembe kabisa katika kulinda upigaji na kuhesabiwa kwa kura. Kumbukeni ushindi wa Busanda utapelekea ushindi Biharamulo. Chondechomde msibweteke.

Last time Mbeya vijijini mliboa kwa uzembe wa kipuuzi.

Wana JF wapenda mabadiliko tuwashauri hawa washinde Busanda. Mawazo yenu please.
 
pia wawe karibu na wananchi na kuwaelimisha zaidi, mfano kuweka tv kwenye stategic position na kutangaza sera zao hata kwa kutumia generator na kuonyesha ubaya wa uongozi wa ccm, wa uwaibia rasilima na kuwapa kiduchu ili kuwadanganya, pia kutokuwa nma maendeleo kutoka na uongozi mbovu wa ccm, ukija uchaguzi ndio wanajifanya kila kitu kiko katika mipango blah blah, njia nyingine ni kuwaelemisha watu kama sokoni na wanafunzi walio na umri wa kupiga kura, na hata waalimu ambao miaka nenda miaka rudi hawathaminiwi na ccm, ila wakati wa uchaguzi
 


sure, kama vile wahubiri injili tunavyofanya!
 
Ushauri mwingine: CCM wanapita wanatangaza kuwa wananchi wasikaribie helikopter ya CHADEMA kwani itawalipukia kama mabomu ya mbagala, sasa hapa ndipo pa kuwapatia CCM " JE CHADEMA WAKISEMA KUWA CCM WALILIPUA MABOMU MBAGALA MAKUSUDI ILI WAWATISHE WANANCHI WATAKUWA WAMEKOSEA?" Ikumbukwe kuwa watu walikufa kule Mbagala sasa hii ni busara kwa CCM kutumia tukio hilo lililotokea wakati wao wakiwa wanacontrol jeshi kuwatishia wananchi?

 
Kama ni kweli kwamba wana CCM wanawashauri watu wa Busanda wasikusanyike mbele ya helikopta kwa sababu italipuka basi wamefilisika kisera zaidi ya nilivyokuwa nafikiria.
 
Kama ni kweli kwamba wana CCM wanawashauri watu wa Busanda wasikusanyike mbele ya helikopta kwa sababu italipuka basi wamefilisika kisera zaidi ya nilivyokuwa nafikiria.

Ndugu yangu umechelewa kulijua hili....
 


,,,Yote kwa yote,hawa wapinzani wangekua wanaumoja wao,hakika MNYAMA angeangukia PUA safari hii,manake hali ni mbaya kweli,kuanzia huko KATORO mpaka hukoo UNGUJA katika jimbo la MAGOGONI,tatizo wao ndo wanazigawa KURA hawa wapinzani.
 
,,,Yote kwa yote,hawa wapinzani wangekua wanaumoja wao,hakika MNYAMA angeangukia PUA safari hii,manake hali ni mbaya kweli,kuanzia huko KATORO mpaka hukoo UNGUJA katika jimbo la MAGOGONI,tatizo wao ndo wanazigawa KURA hawa wapinzani.
Asante kwa kuliona hili, huu ndio ungekuwa ushauri kwa chadema waachane na umaarufu wa chama, waangalie kukubalika kwa mgombea wao, kama yuko juu ya wa cuf, waishauri cuf ivunje kampeni, wajiunge na Chadema. Na kama ni mgombea wa CUF yuko juu, Chedema wavunje kambi. Yaani Busanda ni ushindi wa wazi wa wapinzani ila mgawanyo wa kura za Chadema na CUF, yaani kitendo cha Chadema na CUF kuvutana ili kupokonyana Busanda, kutapelekea jimbo hilo kuwaponyoka wote na kudondokea mikononi mwa CCM.
 
eee bwana haya ndiyo maneno ila sisi wote tujitahidini kufichua njama za uibaji kura tu ndio unaotuangusha maana, last time hapo arusha wasingepata hata mmoja si huyu wa mjini wala arumeru. kilichotumika ni masunduku yaliyojaa yametangulizwa kwa hiyo tukakosa. sijui tutafanyaje wtz jamani hee wanatuibia hata kura mbali na pesa.
 

Shida kubwa ya Mbeya Vijijini ni kwamba mgombea

aliyekuwa chaguo la wanaMbeya na wanaMageuzi, kijana

kipenzi wao, Sambwee Shitambala Gaya alitolewa katika

hatua za mwisho kabisa baada ya kudaiwa kujiapisha kwa

kutumia kampuni yake ya uwakili, badala ya kwenda

mahakamani.

Matokeo yake ni kwamba wananchi walisusa hata kwenda

vituoni kupiga kura.

Wazo ulilotoa bwana KANIKI WA 1974 ni la msingi sana.

Bila kufanya hivyo, MNYAMA ATASHINDA KWA KISHINDO!
 
Hivi hawa vibarua wetu wa TBC1 wanatutaka nini Watanzania? Mbona wanazidisha kuwabeza wazalendo wa Chadema katika nchi yetu kwa kujaribu kuwajengea picha mbaya kwa Watanzania? Haki ya nani siku yao itafika tu.
 
i wish all the Best to Chadema na MUNGu anayeipenda TANZANIA atawapa ushindi wa KISHINDO
 
i wish all the Best to Chadema na MUNGu anayeipenda TANZANIA atawapa ushindi wa KISHINDO


Tupom pamoja ndugu. Mungu isaidie chadema au kama cuf sio mbaya kivile ili mmoja wao ashinde
 
mimi hata kama angekuwa panya bora ashinde hicho kiti kuliko CCM!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…