Astaghfirullah llahu al adhwim, alladhi laa ilaha illa Llah, al hayyu al qayyum.
Nafurahi kukubaliana nami kwamba Maalim hajamuandaa na kumtambulisha mrithi wake na time is not on his side.
Kama chama ,Maalim Seif kaandaa makomred wa kutosha watakao fanana na yeye ,pindi akistaaf au kupatwa na faradhi haitakuwa mwisho wa siasa za Kupigania Haki za Zanzibar,
kweli pengo litakuwepo lakini litazibwa kwa wengine wengi wa mfano wake.
Hii ni taasisi ,huwezi kumuandaa mtu wako makhsusi ,kufanya hivyo itakuwa usultani huo, bali itategemea Kura za wajumbe na watia nia watakaochukua fomu ya kuwania kiti chake pale atakapokuwa hayupo
Kwa hiyo usijali.
Akina sisi tulimjua Maalim tukiwa wadoogo, na Kumpenda na kumfuata na kujifunza mengi kwake
Leo na sisi tumeshakuwa na kutamani tuanze kazi ili nasi tuoneshe uwezo wetu, lakini si kwa Uwepo wake akiwa Kazini, bali tutasaidiana nae kwa sasa bega kwa bega kuendeleza harakati huku tukijua tuna mwega pembeni ,mtu mwenye karama nyingi tuu.
Bado tunamuamini na Tunaimaninaye kwa kuwa hajawahipo kutusaliti, na naamini hatofanyapo hivyo.
Yeye ni sehemu katika Nyoyo za watu kisiasa Zanzibari