Ushauri kwa Diamond kama shabiki beef halikusaidii tumia akili kulikwepa

Ushauri kwa Diamond kama shabiki beef halikusaidii tumia akili kulikwepa

Katoa nyimbo 3 zikabuma akaona atafanyaje sasa na hasimu wake amelala hakuna mpambano akaamua kuchokoza vita jamaa aaamke na kilichotokea jamaa ameamka kweli kweli na kwa nguvu zote na diamond kajikuta anafeli vibaya sana
Lkn tukiangalia sio kwamba amefeli sana kiivyo kama unavyosema mkuu, tatzo ilizoeleka yeye ni champion siku zote this time kiba naye kawa champion but still I say Diamond is the best, anatakiwa tu areset tricky zake
 
Yaaani huoo ndio ukwelii, jamaa mi kanikera sanaa
Haikua na sababu yeyote ya kutoa hiyo ngoma mdaa huuu angali terehe 1,anataka aachie ngoma na patorank
Mimi kma shabiki wa Diamond, nasema izo stress sake asituletee mashabiki ,maana mpka sasaa atuelewi ipi tuipe msukumo, yaa ZILIPENDWAA au Hiyo ya tarehe 1.
Umeewapa wapinzani nguvu, na promo ya kutoshaa bilaa sababuu
Huh ulilfnyaa ni ujingaa. [emoji22]
 
Naomba mods msifute thread yangu au kuiunganisha.
Ww diamond ni msanii mkubwa sana na ulikuwa umejijengea heshima kubwa sana kwenye jamii kutokan na kazi zako za mziki. Ni mtu ambaye ulikuwa una deel na kazi zako tu, ulikuwa siyo mtu wa mabifu na maugomvi mtu mnyenyekevu nakumbuka wasanii wenzio walikuwa wanakusem sana lakini ulikuwa unapiga kimy na kazi ndo zilikuwa zinaongea zenyewe.
Lakini kwa nini umebadirika ghafla maana siyo yule mond niliyemzoea umekuwa mropokaji, mtaka shari, kutukana na kudharirisha wanawake, uku ukijua kabisa hawo ndo mafansi zako wakubwa. Kitu kingine ambacho sijapendezwa nacho ni hii tabia ulioianzisha ya kutaka uonekane ww tu hutaki wenzio wasikike, inajulikana kabisa ww na kiba haziivi na maadui zako wameunganish nguvu na kiba ili wakuumize kwa nn unashindwa kujiongeza na kutumia akili kujitenga na hilo beef, sikuona umuhimu wowte wa ww kuamua kuiblock ngoma ya mshindani wako kwa kuachia wimbo mda mchache baada ya yeye kutoa wimbo., Inajulikana kuwa tar 1 sep unatoa wimbo uloshirikiana na patoranking si ungesubiri muda ukafika ukatoa huwo wimbo. Na jinsi wimbo wa kiba ulivo mbovu ungekuw tyar ushajifia lakini cha ajabu umekurupuka ukatoa wimbo ambao ni mzuri tu lkn watu tumeuchukia kwa sababu umeutoa ili kuu block wimbo wa kiba usivume kitu ambacho ni ushamba na unprofessional na badala yake imeback fire kwako, kama mtu wa kujifunza umejifunza next time usirudie, fanya kazi zako ww kama ww na siyo kwa mashindano. Beef halikufaishi ila linamfaidisha mpinzani wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiba hajawahi kuwa mpinzani wa domo ila domo ndio analazimisha upinzani na king...

domo anaugulia rohoni kutokuheshimika kwake ukilinganisha na heshima anazozipata king.

Ushauri wako ni mzuri ila ongezea kwamba domo anahitaji kupunguza siteresi za zari kuwa bize na wanawe na kumwacha yeye awe bize na vicheche kwa KUSOMA VITABU na sio kukaa na vitoto vidogo visivyoweza kumpa mawazo ya kiutu uzima ukichukulia ni mlezi wa watoto 6 sio mchezo.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Hivi tarehe moja bado siku ngapi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
1.5 M views
Bado kwaya ya WCB hawajafikisha 1 M views
4dc85d70e843e334ebf6bb03881294fe.jpg


838abfb5bc7befbc8781ec11012269de.jpg
 
Binafsi ni shabiki damu wa Diamond pamoja na kwamba huwa napata wasaa wa kusikiliza kazi za wasanii wengine nje ya WCB ili kuonja radha tofauti ya bongo Fleva.
Diamond kafanya mengi ya msingi na muhimu katika tasnia hii ya burudani, Diamond kaiambia dunia kuna nchi Inaitwa Tanzania ina mziki wake unaitwa Bongo Fleva na dunia ikapokea kwa mikono miwili kile ilicho ambiwa na Diamond.

Sio unafiki, wasanii wengi walikata tamaa na huu mziki, hata huyu Kiba wa Cinderella, Msiniseme, MC Muga na nyinginezo alikata tamaa na huu mziki ni Diamond alive mrudisha kwenye game.

Diamond Kama ilivyo kwa akina Sugu, Prof Jay, Solothang, na wakali wengine aliwaaminisha wazazi wengi Kuwa BongoFleva siyo uhuni, aliwashape vijana wengi waichukulie fani hii Kama kazi ambayo inaweza wajengea heshima na kuwapa kipato cha kuweza kutengeneza kesho yao na familia zao. Binafsi Nina mkubali sana huyu kijana, kuna wakati nilitamani hata mwanangu nimpeleke kwenye shule zinazo toa elimu ya Music, lakini hiki anacho anza kukifanya hivi karibuni sio tu kinakatisha tamaa bali kinafedhesha.

Diamond anatufedhesha Mashabiki na wapenzi wa sanaa yake, sijajua haya mabadiliko yanatokana na nini ukizingatia anaofanya nao kazi sasa, ndio hao hao waliomfikisha hapo!
Diamond wa leo anashindwa itumia vyema mitandao ya kijamii kama alivyokuwa akifanya awali, kuna kipindi aliwahi mtuhumu Wema kuwa anapenda sana kuweka mambo yao ya faragha hadharani binafsi nilimuelewa sana, leo anafanya yale aliyokuwa akiyachukia kipindi cha nyuma!

Pages za Diamond kwenye mitandao ya kijamii zilijaa kazi, leo yupo States, mara yupo London kesho yupo SA, hii ilikuwa inatupa Motisha kuwa Mwenyezi Mungu anabariki kazi ya mikono ya huyu kijana. Lakini leo hii Diamond kawa wa kupost MATUSI KWENYE KURASA ZAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII!
Mimi sitaki zungumzia alichofanya hivi karibuni dhidi ya mshindani wake ambaye mimi binafsi siamini kama ni mshindani wake (Diamond akirudi kwenye my number one, nataka kulewa na kutupa radha ile ya Tatizo kwetu Mbagala, Nitarejea sioni mshindani wowote kati ya hawa vijana)
Diamond alimuacha mbali sana Kiba, leo hii kaamua kumfanya Kiba mshindani wake kwa makosa madogo ambayo yanarekebishika lakini kinyume chake yeye anapalilia hayo makosa.

MFANO:
Diamond siyo wa kwanza kupewa skendo za kuzalisha mabinti na kukataa majukumu, na akumbuke yeye siyo mume wa Zari labda kama tumefichwa, lugha aliyoitoa dhidi ya wanao mshutumu kukataa majukumu yake kwa Hamisa imechefua walio wengi sana hasa wanawake ambayo ndio wapenzi hasa wa BONGO FLEVA.

Diamond amesahau ama hajui HULKA YA MWAFRIKA KAMA SIYO MTANZANIA kuwa hapendi kuona kiwango cha mafanikio ya MTU na hasa kama anafahamu yeye ndio sababu ya wewe kuwa na mafanikio hayo. Watu wa namna hii hupenda kukuonyesha kuwa wao ndio kila kitu katika maisha yako na ukitaka kuwaonyesha kuwa ni BIDII YAKO KATIKA MAISHA wataanza kukutengenezea visa waku_prove wrong! Na nini ndicho wanachofanya Watanzania dhidi ya huyu kijana. Diamond alipaswa kuweka kando maisha yake binafsi, lakini hili nalo mdogo wangu hajaliona.

Ofisini:
Bila kupepesa macho, Prodyuza wa WCB Ndugu Laizer kaelemewa, ana majukumu mengi sasa WCB ina member sio chini ya 6 na hawa wanategemea ubongo wa Laizer ufanye ubunifu wa kimataifa kama alivyofanya na anavyofanya kwa Bosi wao! Hili jambo haliwezekani. Diamond sishauri umkimbie huyu kijana mwenzio bali muongezee nguvu, mtafutie MTU wa kumsiadia baadhi ya vitu kama mixing na mengineyo, lakini pia sio mbaya kama ukiwachukua marodyuza wakali kama Mika Mwamba, Master Jay, Enrico na kuwaomba waje wakufanyie kazi kwenye ofisi zako.
Chunguza melody na vionjo vya kazi zenu karibia nyingi sasa mnafanana hii inachosha na inaudhi mashabiki.

Management:
Sitaki Mzungumzia sana Tale huyu ni mswahili kama waswahili wengine hasa nikiliangalia kundi la Tip Top Connection, mtazame Salam sijajua kapatwa na nini ila binafsi naona kama naye kalewa MAFANIKIO YAKO, ama kuna jambo nyuma ya pazia. Diamond sijasikia mashudu ama mapovu toka kwa Binti Seven Mosha juu ya hili bifu lenu, unadhani hakupondi?
Lakini tazama anachofanya Meneja wako anakuchoresha sana, anakuingiza kwenye kumi na nane za wakuchukiao 100% jaribuni kuliepuka hili.

Please nakuomba hiyo Tarehe 1 September usilete uswahili fanya kazi kama zamani haya mengine waachie mashabiki waamue SIYO kama anavyosema Meneja na wakati huo huo anafanya upumbavu
Aisee umeongea ukwelii kabisaa
Ilaa jamaa ametupa fedheha sana. ...!

Kiufupi yaani stress zake asituletee na sisi, Alafu kila kitu kibayaa sikuizi anasemwa yeyee, na kwanini iwee yeyee (kunavingine vinakua na ukweli, ilaa anapotezea na neneo kiki) hii I natupa fedhehaa sanaa sisi tunao mpa support kwa mapenzi yetu.

Kuzungumziwa sio kitu kibayaa, ilaa azungumziwe kwa mazurii, na hata mabaya yakitokea yasiwe hivyoo.. Maana hakuna alive kamilika.

Kiukweli anatuchoshaa sanaa, Apige kazi kwa namna ambavyo tumemzoeaa. Sio maneno ya hovyo hovyoo tu. [emoji21] [emoji21]
 
Ndo maana namshauri japo sijui kama wanapitaga kwny iz forum. Apunguze mihemuko na kumuwaza sana mshindani wake awaze kazi zake zaidi alafu atumie akili kubwa kujitenga na hili beef maana linamfaidisha mpinzani wake kuliko yeye.

Alafu kama ingekuwa ni maamuzi yangu sallam sk inatakiwa afukuzwe pale WCB maana ndo naona anachochea sana maugomvi siyo mtu wa amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna cha kumfaidisha mpinzani wake, kiba anafaidishwa na mzki wake mzuri unaopendwa na wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemshauri vzr sana. Kifupi yaan yeye kasababisha kupaisha wimbo wa kiba bila kujua. Angekaa kimya wala isingekuwa hivi, ameonekana kama kapaniki hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yule hana akili, kwanza sijui nani aliemwambia atoe ile remix ya fresh, hapo ndo aliwafanya watu wakaweka attention kwa Kiba. Sasa kiba alivyotoa wimbo wake, domo akapost insta picha ya mtu anacheka. Within few hours akaachia ngoma na yeye. This is unproffesional kabisa kwa mtu kama yeye. Ujinga mwingine bwana taabu tupu.
 
Ngoja waje ..alafu walifikiri jamaa atatoa vijembe Kama ilivyo jadi yao ! Chakushangaza Sasa jamaa katoa kitu tofauti ..duh Walivyofikiria sivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah ni vyema kama hakizi vigezo lzm afukuzwea sk anapenda san vita ni mtu wa vijembe sana vitu vinavofanya kuongeza chuki kwa mashabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sk ndio chanzo cha beef la domo na dimpoz...mwarabu koko yule mbeambea na majungu ya kuswahili basi jipya hana anamtia shimoni domo wa watu....ifike pahala afutwe ajira na mwenzake tale iingie timu mpya....vigezo vya elimu kwa manager vizingatiwe tafadhali....vyetiiii...vyeti jamaniiii.....ugangauganga hauna nafasiiii...ELIMU...ELIMUUU...ELIMUUUUU

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Mi mpaka ss cjaona hoja humu zaidi ya vijembe tu kwa sababu wote wametoa ngoma na zote ni kali na naona huyu chibu ndo katoa kali zaidi , manake yy amekuwa ni mtu anaeonyesha kweli yy ni msanii kwani anaimba atleast kwa kubdilikabadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi mpaka ss cjaona hoja humu zaidi ya vijembe tu kwa sababu wote wametoa ngoma na zote ni kali na naona huyu chibu ndo katoa kali zaidi , manake yy amekuwa ni mtu anaeonyesha kweli yy ni msanii kwani anaimba atleast kwa kubdilikabadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama huko kwenu ni usiku kama huku kwetu tandale..KOJOA UKALALEE.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 

Attachments

Tusi liko wapi?!!kaahhh!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia upya ulichokoment apo juu...huu uzi unamuhusu mond na mashabiki zake ni jinsi gani anatakiwa kuyakabiri aya majanga yanayomkumba so ww kama huna cha kushauli bora ukapita iv.......na kama unatak kuwatusi watu nenda kwny nyuzi zenye kariba iyo.

Am done.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom