Ushauri kwa Diamond Platnumz na kundi la WASAFI

Ukihudhuria shoo za wasanii wa bongo usisikie maneno haya basi amini Sio bongo!

Sema woyooooo woyo woyooooo!

Twende hivi twende hivi......


Siwasikii siwasikii......
 
hivi wale wasanii wamarekani waliowahi kuja kwenye fiesta waliimba live?
 
Huwa inashangaza pale msanii anakuwa anaimba, anakatisha kuimba halaf anaelekezea maiki kwa mashabiki ili waimbe.

Ghafla msanii anaanza;

Piga keleleeeeee
Piga keleleeeeee
Piga keleeeeeee
Piga keleleeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umeanza vizuri nikajua ni mshauri wa kweli....ila ulipoandika matamsha yenu yanaboa nikajua tayari ushatumwa na Team Kiba.
 
Umeanza vizuri nikajua ni mshauri wa kweli....ila ulipoandika matamsha yenu yanaboa nikajua tayari ushatumwa na Team Kiba.
Hiyo ndiyo Tanzania yetu. Ukitoa ushauri kwa serikali utaambiwa umetumwa ba mabeberu. Ukitoa ushauri kwa Ali Kiba utaambiwa wewe ni timu Diamond.

Huwa sielewi kwa sababu gani huwa tunashindwa kuwa kwenye mada.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

umeandika nini??

live diamond na wenzien hawawezi, diamond hata kukuimbia weemwe sebuleni bila vyombo hawezi

mkuu acha kujiaibisha
 
Wengine ndio raha yao kuimbishwa na ndio sababu hata wengine wanavuka mipaka hadi kuwashika hao wasanii makalio na mpaka kule kwa Babu.
Wenyewe eti wanaita "KUCHIZIKA", kwani mizuka kama hiyo hua haikupandi Shadeeya unapopagawishwa na wimbo unaokugusa sana?πŸ˜€πŸ˜€
 
Acha uongo,tumeshuhudia akina busta ryhmes,TI wakiafanya makubwa show za kufunga fiesta miaka ya nyuma!!!!
Angalia show za Fally Ipupa utaelewa mtoa mada anamaanisha nini!
 
Acha uongo,tumeshuhudia akina busta ryhmes,TI wakiafanya makubwa show za kufunga fiesta miaka ya nyuma!!!!
Angalia show za Fally Ipupa utaelewa mtoa mada anamaanisha nini!
Ktk Fiesta zote Busta pekee ndiye aliyefanya vizuri huyo TI alifanya hovyo na wote walitumia play back.Wasanii wa nje waliopiga na live band ni Shaggy na Sean Paul, ila show ya Shaggy ilikuwa kali kuliko ya Sean Paul.
 
Hakuna kitu sipendi kama niende tamashani alafu nisikie "mikono juu" au ile mwanamziki anakaa kimya anasubiri mashabiki waimbe...naweza kutoka pasipo majuto yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwanini tanzania yetu ukimshauri mtu unaonekana una chuki naye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…