[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] inaonekana wewe ni muhudhuriaji mzuri...Ukihudhuria shoo za wasanii wa bongo usisikie maneno haya basi amini Sio bongo!
Sema woyooooo woyo woyooooo!
Twende hivi twende hivi......
Siwasikii siwasikii......
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] inaonekana wewe ni muhudhuriaji mzuri...
Usiende mbali hapahapa bongo Christian Bella kwenye show sake akiwa na bendi huwa anaimba peke yaka masaa mawili na zaidi mnamsikiliza yeye tu hata wazaire kwenye show zao huwa wanawaambia mkae msikilize masauti hao madomo hawana pumzi za live!!....Mbona maelezo yako haya yanaonyesha na hadi kuthibitisha kabisa kwamba Wewe siyo Mhudhuriaji na Mfuatiliaji mzuri wa Miziki hasa ya ( Live ) Mubashara kabisa? Hebu rudi tena kaa chini halafu fanya ' assignment ' yako vyema hasa kwa hao Wanamuziki wa huko Mamtoni ( Marekani / Ulaya ) uone kama hawafanyi kama akina Diamond na labda kwa kukusaidia tu ni kwamba hata hawa akina Ndomo ( Diamond ) na Wasanii wengi wa Kibongobongo nao hivyo unavyoona wanafanya ' Stejini ' kwa 100% wanawaiga hao hao ambao umewatetea kuwa huwa hawafanyi hivyo. Halafu Siku zingine acha Kuzunguka na ukweli ni kwamba una ' Chuki ' zako tu Ndomo ( Diamond ) japo umejitahidi mno kuwa ' very diplomatic ' katika ' Content ' yako nzima ya ' Uzi ' ili tusikushtukie.
Napenda kusema kuwa nampenda sana Diamond platnumz na nyota wote wa kundi la WASAFI.
Pia nawapenda nyota wote wa muziki wa Tanzania wakiwamo Navy Kenzo na Ali Kiba.
Nimekuwa nikisikiliza na kutazama muziki wa Tanzania kupitia YouTube na internet maana niko nje ya nchi.
Sijawahi kuhudhuria live performance ya Diamond Platnumz ama ya mwanamuziki yeyote yule wa Tanzania.
Kwa kutazama na kusikiliza records za Diamond Platnumz na wanamuziki wengine, muziki unavutia sana.
Lakini pia nimekuwa nikitazama videos za live performance za Diamond Platnumz.
Hapo awali nilidhani kule kukatisha katisha kuimba kila baada ya sekunde chache wakiwa jukwaani na kuwahamasisha watu waimbe ni editing tu. Kumbe ni halisi. Nimegundua baada ya tamasha ya WASAFI la Nairobi kulalamikiwa sana na waKenya.
Naomba Diamond Platnumz na nyota wote wa muziki wa Tanzania.
Jifunzeni kwa magwiji kama Michael Jackson na wengine namna bora ya live performance.
Wao hutumia muda mwingi kuimba na kucheza bila kukatisha na kutaka watu ndiyo waimbe. Ni mara chache sana hufanya hivyo.
Matamasha yenu yanaboa.
Iweje watu walipe kuja kuwaona mkiimba na kucheza live, mnaishia kuruka ruka na kutaka mashabiki ndiyo waimbe.
Msipojirekebisha mtapotea kwenye muziki.
Asanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app