Ushauri kwa IGP: Ukitaka uwazi katika uwajibikaji wa Polisi ruhusu wawe wanarekodiwa na Raia hata ndani ya kituo cha polisi

Hata video zikiwepo hakuna lolote litakalofanyika. Kama kuna video za ngono za wanasiasa na bado wana nafasi zao mnafikiri video za polisi zitawafanya wawajibike?
 
Nikikuta polisi anapigana na jambazi, namsaidia jambazi tumuue polisi. Halafu namshauri jambazi aache uharifu. Akifanya uhalifu namuitia mwizi.
 
Hakuna sababu ya kurecord, zifungwe CCTV camera mpaka mahabusu na maeneo yote ya polisi
 
Hilo hawezi.Na kwa kweli sio hawezi bali HATHUBUTU maana ndio mfumo uliomlea
 
Ni hatari kurekodi maeneo nyeti bro
Maeneo nyeti yapi, vituo vya polisi au?
Kuna unyeti gani wakati hapa nilipo naweza kuangalia hadi ikulu kwa msaada wa teknolojia?
Hakuna maeneo nyeti. Haya ni maeneo ya umma na tunapaswa kuchukua video mambo yakiwa hovyo
 
Kupiga ni iwapo umekataa kutoa ushirikiano, sio hiyo ya kupiga ili kumtia mtu hofu akiri kosa ambalo hajatenda, ama kujiwekea mazingira ya kupata rushwa. Kwasasa polisi wetu wanachojua ni kupiga tu pindi wanapokamata mtuhumiwa jambo ambalo si sahihi.
Na polis huwa hawawezi tu kuanza kupiga bila kumletea ukinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…