Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Nianze Kwa kumuunga mkono Mbunge wa Viti maalum Iringa Jesca Msambàtavangu juu wa utendaji wa wizara ya Jinsia na watoto pamoja na Idara zake jinsi zilivyojikita kutetea upande mmoja WA wanawake na watoto wa Kike pekee.
Afande IGP, ugonjwa huu umelikumba Kwa kiwango kikubwa Dawati lako la jinsia na watoto nchini. Kwanza Kwa sehemu kubwa watendaji wake ni wanawake (Askari wa kike) na karibu mikoa yote niliyotembelea naona viongozi wake ni wanawake. Kama Dawati linashughulikia jinsia Kwa nini liegemee sehemu moja? Niko tayari kukosolewa kama kuna mkoa Mkuu wa Dawati ni Mwanaume.
Hali hii imesababisha wanawake kuonekana ndio Wenye haki pekee kwenye madawati haya. NI kweli jinsia Ke ilikuwa chini Kwa Muda mrefu lakini siku zote unapoegemee kuinua upande mmoja pekee elewa unadidimiza upande wa pili.
Anachoongea Msambatavangu ni Uhalisia wa utendaji katika Madawati ya jinsia Polisi. Wanaume na watoto wa kiume ni binadamu wa daraja la pili Kwa huduma.
Najua umakini wako pale unapoweka siasa pembani, hebu angalia muundo na utendaji wa kitengo hiki ili kunusuru mustakabali wa Mtoto wa kiume ambaye anaegemewa kuwa kichwa cha nyumba mbeleni.