Ushauri kwa ITV

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kwanza kabisa niipongeze Kampuni ya ITV kama channel pendwa. Niwashirikishe changamoto inayoikabili ITV.

Kipindi cha taarifa ya habari ni kipindi muhimu sana kwanza inatazamwa na karibu wananchi wote wa Tanzania na Afrika Mashariki lakini baadhi ya watangazaji hawaitendei haki kipindi hiki.

Mfano kuna mtangazaji mmoja ambaye ni mwana Mama siyo maakini wakati anatangaza taarifa ya habari. Kwanza hana concetration wakati wa utangazaji na hana flow (mtiririko mzuri) wakati wa kipindi hiki.

Niwapongeza wengine ambao ni watangazaji wazuri kama F. Middle, Odana Madai na wengineo. Ni vema kila mara wawe wanapelekwa kozi fupi fupi ili kumarisha utendaji wao wa kazi.
 
ITV suuuper Brand...Afrika Mashariki
 
Shida ingine wanasoma habari mbio mbio sijui huwa wanakimbilia wapi? Wajifunze kwa wenzao wa Azam. Angalau TBC wamebadilika kidogo japo UCCM ndo donda sugu linalowasumbua.
 
Pia habari za kimataifa waende kama star tv sio east Africa tu
 
Halafu tabia ya sauti na picha kukata kata wakati wa habari ni kero ya muda mrefu sijui hawalioni hili pia?
Pia habari zao zipo too shallow hazipo deep wanakimbia kimbia tu utadhani wapo kwenye riadha na muda.
Ni bora watoe habari 3 kwa kina kuliko kutoa habari 20 shallow.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Shida ingine wanasoma habari mbio mbio sijui huwa wanakimbilia wapi? Wajifunze kwa wenzao wa Azam. Angalau TBC wamebadilika kidogo japo UCCM ndo donda sugu linalowasumbua.
Jambo jingine la muhimu sana, sasa umefika wakati waifanyie 'Make up' studio yao. Miaka Nenda rudi muonekano wa studio yao uko vile vile. Ni aibu sana ITV mnajiita super brand wakati muonekano wa studio zenu ni kama wa miaka 1970, wakati material za 'Formika' zilikuwa zimeingia Sokoni. Sasa karne ya 21 bado ni pambo la studio zenu. Igeni Citizen ya Kenya.
 
Pia habari za kimataifa waende kama star tv sio east Africa tu
Tatizo la habari za kimataifa, source ni nyingi, mfano kuna bbcswahili na ma channel kibao, itv inaona kuitangaza ni kama kupoteza muda maana ni kukopi na kupesti habari za vyombo vya Ulaya, na kusambaza propaganda ambazo mara nyengine sio za kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…