Mtanganyikamimi
Member
- Aug 13, 2013
- 64
- 13
Mimi ni Mtanzania. Ni raia wa kawaida kabisa! Napenda kutoa Ushauri huu wa Jeshi la Polisi.
1. Nalishauri Jeshi la polisi liachane na ushaabiki wa vyama vya siasa. Liache kuingilia shughuli za vyama siasa kama zinaendeshwa kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria za nchi.
2. Jeshi la polisi lazima liheshimu na kumlinda kila raia wa nchi hii bila kujali itikadi za kisiasa, kidini na kabila au ukanda.
3. Jeshi la polisi liachane kabisa na unyanyasaji, udhalilishaji na mauaji ya raia wenye hatia na wasiokuwa na hatia. Jeshi la polisi lazima litambue kwamba halina mamlaka ya kuwahukumu kipigo au kifo raia wenye makosa. kazi yao ni kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vyenye mamlaka ya kuthibitisha makosa yao na hatimaye kutoa hukumu.
4. Jeshi la polisi litambue kwamba kila Mtanzania ana haki ya kuongoza au kuwa kiongozi katika nchi hii kwa njia ya uchaguzi au njia yoyote ile halali. Nawashauri watumie akili zao na utashi waliopewa na mwenyezi Mungu, wapime na watafakari maagizo wanayopewa na watawala ili wawaumize wale wanaowahofia kwamba huenda wakawaondoa madarakani tena si kwa mapinduzi bali kwa njia ya Kidemokrasia. Kumbukeni kwamba hao watawala wanaowatumia ipo siku watawakana.
5. Polisi, kumbuka wewe unaepiga risasi raia, unaepiga mabomu raia na unaepiga virungu raia wa nchi hii na wewe ni raia wa nchi. Ipo siku na wewe utapigwa, au kama si wewe, baba yako au mama yako au watoto wako au mjomba wako au dada yako au bibi yako au babu yako au shangazi yako naye atapigwa na wenzako. Je, utawalaani wenzako!
6. Mwisho kabisa, Aliyesema, "Wapigwe Tu. Tumechoka", naye kama siyo yeye, basi ndugu zake watapigwa tu, kwani wanaopigwa sasa nao watasema wamechoka. Lakini watapigwa na Sheria za nchi, Hawataonewa wala kudhalilishwa, watahukumiwa kulingana na matendo yao.
MUNGU IBARIKI TANZANIA