Ushauri: Kwa kiwango cha mshahara kisichozidi Tsh. 400,000/-, benki inaweza kunipa mkopo wa Tsh. 3,000,000/-?

Ushauri: Kwa kiwango cha mshahara kisichozidi Tsh. 400,000/-, benki inaweza kunipa mkopo wa Tsh. 3,000,000/-?

Suip

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,353
Reaction score
815
Kiwango cha mshahara nilichokuwa nacho baada ya makato yote ni 545,000/= baada ya kuchukua mkopo mwaka juzi wakawa wananikata 147,861/= na kiwango cha mshahara ninachoenda nacho nyumbani ni 397,139/=

Sasa hivi ninahitaji mkopo mwingine wa kama 3,000,000/= ambao kipindi cha kulipa ni miaka 4 na kiwango cha mshahara kwenda nacho nyumbani kitabaki 300,000/=

Je, benki ya NMB itakubali kunipatia huo mkopo mwingine? Na kwa upande wa DED(Mkurugenzi wa Halmashauri) kuna kizuizi cha hiyo take home?

Nisije aibika kabla ya kwenda Benki, mwenye uzoefu tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sera ni kwamba katika makato yako yote ya mikopo ukatwe lakini ubakie na take home kuanzia 50% mpaka 40% ya mshahara wako, kwa hiyo wewe kopa tu mshahara bado mnono huo.
 
Sera ni kwamba katika makato yako yote ya mikopo ukatwe lakini ubakie na take home kuanzia 50% mpaka 40% ya mshahara wako, kwa hiyo wewe kopa tu mshahara bado mnono huo.
Haaaa!!!hapo anatakiwa abaki na 250,000/ ambapo pesa atakayochukua akilia bata ataanza kuiona kazi ni chungu.
 
Nchi hii kuna unafuu kwa awamu hii, mbona kila moja analia,kuanzia wafanyabiashara, wakulima sembuse watumishi wa umma,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom