Ushauri kwa kocha zahera kutokana na mchezo wa leo

Ushauri kwa kocha zahera kutokana na mchezo wa leo

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kama mshabiki nilioufuatilia mchezo wa leo kwenye luninga, wachezaji wako wanafanya makosa ambayo hayawezi kuvumilika. Mfano lile goli la kwanza yule mchezaji anayeitwa Chikupe anafanya faulo dhahiri kabisa kwenye eneo la hatari. Kwa mchezaji mwenye akili pale siyo mahali pa kufanyia faulo.

Nadhani mchezo ujao yule Chikupe usimpange tena. Kwanza ni mfupi na hana mbio kabisa. Goli la pili mpira umetoka mbali na kumpita kipa kwa urahisi kabisa. Pamoja na kutokuwa na makipa wazuri nashauri msimu ujao mumsajili kipa mwenye uwezo na mwepesi. Sikubali Kakolanya arudishwe lakini pia mafunzo ya makipa ni muhimu sana.

Hata hivyo tumshukuru Mungu timu imesonga mbele.
 
Back
Top Bottom