Ushauri kwa mamlaka kwa mikataba yote itakayoingiwa na Serikali siku za usoni

Ushauri kwa mamlaka kwa mikataba yote itakayoingiwa na Serikali siku za usoni

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Poleni sana. Mkataba wa DP World imetufumbua macho hata sisi wananchi wa vijijini.

Ni ushauri kwa Mamlaka. Mikataba yote itakayoingiwa na Serikali katika siku za usoni ijumuishe Watalaam wafuatao:

1. Wanasheria wabobezi kutoka TLS na ZLS.

2. Wanasheria toka Sekta binafsi.

3. Wachumi toka Vyuo Vikuu vya nchini na Sekta binafsi.

4. Wahandisi wabobezi kama mkataba ni wa kihandisi.

5. Wale wote watakonekaana mikataba inawagusa.

Nchi ni yetu sote. Tusiingie kwenye mikataba kwa kificho. Mamlaka ijifunze kutokana DP World jinsi ilivyoleta taharuki.

Nawasilisha.
 
Good Advice !!! Though I'm Sure, Someone, Somewhere Is Saying "Who The Hell Do You Think You Are To Say That"?
 
Ktu ya dili haitaki ushiriki wa namna unavyopendekeza
 
Good Advice !!! Though I'm Sure, Someone, Somewhere Is Saying "Who The Hell Do You Think You Are To Say That" !!!???
Na hilo ndilo tatizo la waliopewa madaraka, hawajui wenye mamlaka ni wananchi!
 
Mimi naona katiba ndiyo itatatua haya ya mkataba mibovu.katiba iruhusu kumshitaki rais anapovurunda kama hili la dp world na BANDARI.kwa katiba ya sasa inamfanya rais awe kama hawezi kukosea.lolote atakaloamua lazima litekelezwe na washauri huwa wanamshauri kulingana anavyotaka yeye.ukijifanya kumshauri kwa kukosoa jinsi alivyotaka yeye ataanza kukunanga na kukufukuza kama alivyofukuzwa spika job ndugai na balozi kipilimba
 
Back
Top Bottom