Nimeona kupitia luninga Wahe. Madiwani wakijadili juu ya uanzishwaji wa Wilaya nilizozitaja hapo juu ya Kisesa na Katoro.
Binafsi naishauri Mamlaka inayohusika kuacha kuanzisha Wilaya hizi kwa sababu zifuatazo:-
(1) Watueleze wametumia vigezo gani kuanzisha Wilaya hizi.
(2) Wilaya ya Kisesa itamegwa kutoka Magu, Misungwi, Ilemela, Nyamagana. Tuanze na Wilaya ya Magu. Kwanza Magu sehemu kubwa ya Wilaya ya Magu imemegwa kwenda Busega na sasa Wilaya ya Magu imebaki sehemu ndogo sana na senta kubwa iliyokuwa inategemewa na Magu ni Kisesa.
Hii ina maana Serikali inataka kuiua Wilaya ya Magu jumla. Magu itabaki kama Tarafa. Pili, Kati ya Wilaya zilizo ndogo kabisa katika Mkoa wa Mwanza ni Wilaya ya Misungwi. Wilaya ya Misungwi ikimegwa itabaki kama Kata. Ukipunguza maeneo ya Ilemela, Nyamagana ambazo ni Wilaya ndogo kabisa sasa watabakia na nini?.
Tuchukue Wilaya Katoro inayotakiwa kuanzishwa. Kutoka Geita mjini mpaka Katoro ni kilomita kama 20. Hapa patamwegwa Geita vijijini ambapo sasa Geita vijijini itabaki ndogo sana. Vile vile Wilaya ya Biharamulo itabaki eneo dogo sana. Tusikimbilie kuanzisha Wilaya kwanza ni gharama sana na binafsi sioni sababu za kuzianzisha Wilaya hizi.
Tuweke nguvu katika kupeleka huduma za jamii kwa wananchi. Tusiwe waoga tuishauri Mamlaka tukiwapa sababu za kuwaridhisha ya kutoanzisha Wilaya zilizotajwa hapo juu.