Ushauri kwa Mh Samia:Kwa sasa aendelee kuisimamia collective responsibility tu

Ushauri kwa Mh Samia:Kwa sasa aendelee kuisimamia collective responsibility tu

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,832
Huu ni ushauri kuntu na usio wa kimaslahi kwa Mheshimiwa Rais wa JMT.
Tukirejea ukweli na upekee wa namna alivyoingia madarakani bado mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kwa namna ile ile aliyokuwa anawakibika mh hayati Magufuli.
Rais Samia alikuwa ni makamu wa Rais ikimaanisha bila shaka kuwa maamuzi ya taasisi iliyopita ya Urais yalikuwa ni maamuzi ya pamoja yaani "collective responsibility".
hatujawahi kusikia kuwa maamuzi ya Serikali ya Magufuli yalikuwa ni ya Magufuli pekee ...hatujawahi sikia maamuzi flani ya Magufuli hayakuridhiwa na Samia au baraza la mawaziri au kamati kuu ya CCM.YAANI Namaanisha kuwa hatukisikia mkwaruzano wa kimawazo ulio dhahiri.
Akiwa makamu alimeza yote ya Serikali ya mwendazake aliyameza kwa dhana ya collective responsibility.
Kwa muktadha huu naamini hakuna mabadiliko makubwa ya kimsimamo haswa kwa yale yalioyokuwa yameshapitishwa na kukubaliwa na hatimaye kuletwa kwenye public.
Haitaelekwa eti few months ago serikali ilikuwa inakubali jambo flani na likaelezwa kwa umma halafu leo liwe tofauti na kinzani.

Bado hukumu ya awamu ya sita ni ile ile.kwani washika kibendera walikuwa ni Magufuli na Samia.Magufuli katangulia lakini Samia yupo.

Wananchi,wafanyabiashara,wapinzani na wahusika wote wataulizia maswali yale yale yaliyoahidiwa,yaliyosemwa na mliyotekeleza kama Serikali ya CCM.

Utakachopindua tutaamini ni Serikali yenu ile ile imeyapindua kwa kuwa ulikuwa karibu kisheria kwa mtangulizi wako.
marekebisho yote yanafaa kuwa ni marejebisho mliowahi kuyahadili na iwapo kuna marekebisho makubwa basi yatabaki kuwa marekebisho tarajali toka mlipopewa usukani kwa mara ya pili.

bado mazuri ya magufuli yanaendekea kuwa mazuri yako na mabaya ya magufuli yanaendekea kuwa yako.na zaidi bado mazuri ya JK yanaendelea kuwa mazuri yako/yenu na vivyo hivyo mabaya ya JK kwa kuwa usukani ulirithishwa.

Hakuna atakayekwambia haya

Hivyo basi ni vyema kustick kwenye long term plan with very minor ammendiments .

Ni ushauri tu

#Hutaki unaacha
 
Back
Top Bottom