Profesa Kelembe
Member
- Jul 26, 2013
- 5
- 15
Mheshimiwa Rais kwanza nikupongeze sana kwa jitihada ulizozichukua kuhakikisha mashirika ya umma yanalipa gawio kwa serikali.
Tumeona mwaka 2014/15 ni kiasi kidogo tu kilichokuwa kikitolewa kwa serikali na mashirika mengi yalikuwa hayafanyi vizuri,lakini sasa tunaona tunapata hadi Tshs Trilioni moja na milioni mia tano, hili ni jambo la kupongeza sana.
Ushauri wangu upo katika mambo mawili.Kwanza kuhusu Bodi za Wakurugenzi ambazo zimewasilisha Gawio, pili Kuhusu Bodi za Wakurugenzi ambazo hazijawasilisha Gawio.
1. BODI ZA WAKURUGENZI ZILIZOWASILISHA GAWIO
Nazipongeza Bodi za Wakurugenzi ambazo zimewasilisha gawio kwa Serikali.
Kama hizi Bodi zitaongeza spidi fedha nyingi zaidi ya iliyowasilishwa itapatikana. Pamoja na kwamba Bodi ndizo zilizopokea sifa lakini zimebebwa na Menejimenti za Taasisi hizo. Menejimenti zinapokuwa nzuri zinaficha udhaifu wa Bodi hivyo ushauri wangu hapa ni kuwa ili kuleta hari ya utendaji kwa Menejimenti na kuongeza kasi ya kazi mabadiliko ya kiungozi kwa Bodi ambazo ziomemaliza muda wake hayaepukiki,wanaweza wakarudi viongozi wawili au wa tatu wa Bodi ya zamani.
Wakati mwingine kunakuwa na migongano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ambayo inapunguza hari ya utendaji kazi wa menejimenti hivyo Bodi hiyo inapomaliza muda wake Menejimenti inapata ahueni lakini baadae wanasikia Bodi ile ile imerejeshwa kwa miaka mitatu mingine ina wapunguzia spidi.
Kubadilisha Bodi na kuteua Bodi mpya kunaongeza kasi ya uwajibikaji kwa wakurugenzi kutaka kufanya zaidi ya Bodi iliyopita hivyo tija inaongezeka.Bodi mpya itaweka malengo makubwa zaidi ya Bodi iliyopita hivyo mabadiliko ya uongozi mara nyingi yanaleta mafanikio kuliko kufanya kwa mazoea yale yale kwani Bodi mpya zitakuja na mbinu mpya.
Wapo baadhi ya wajumbe kwenye Bodi hizi ambazo zimewasilisha gawio wapo pia kwenye Bodi zingine mbili au tatu ambazo zimeshindwa kuwasilisha gawio na zingine zimekuwa hazifanyi vizuri .
2.BODI ZA WAKURUGENZI ZISIZOWASILISHA GAWIO
Bodi hizi zimekuwa ni mzigo kwa Serikali,ushauri wangu uzifukuze badala ya kuwaonea huruma na kuwapa muda zaidi ambao wataendelea kuturudisha nyuma kwani walikuwepo muda mrefu na walikuwa na muda wa kutosha kukabiliana na changamoto za taasisi zao hivyo nashauri uzifukuze uteue Bodi mpya zitakazokwenda kuongeza kasi ya kazi na kuwasilisha gawio kwa Serikali.
Mwisho nakutakia afya njema na uendelee kuchapa kazi bila kukatishwa tamaa na mabeberu wa ndani.