Kwanza Salamu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Rais ukiona asilimia kubwa ya wananchi wanapiga kelele kwa jambo la msingi uelewe kuwa kuna jambo linalohitaji kufuatiliwa.
Suala la tozo kwenye miamala za simu limekuwa kubwa na unatakiwa ulitolee/ulichukulie uamuzi wa haraka. Pamoja na nia nzuri ya tozo ya kujenga madarasa, mahopitali, Tarura, vituo vya afya, barabara, mabweni ya wasichana kila Mkoa bado kuna walakini mkubwa katika tozo. Kwa nini utekelezaji wa miradi hii ifanyike kwa mwaka mmoja?
Serikali ipo, watu wapo kwa nini isifanyike kwa awamu. Mafuta yamepanda sana haya yote yanamlenga mwananchi huyo huyo. Mwaka jana mafuta yaliuzwa mpaka Tshs.1800 kwa lita leo hii mafuta yanauzwa kwa Tshs.2,400 tofauti ya Tshs.600.
Jirani yetu hapa Kenya leo wanauza mafuta kwa Tshs2,200 lakin sisi bei yetu bado iko juu. Mhe. Rais tozo hizi zitawafanya watu waichukie Serikali yako na hivyo Mhe. Rais unatakiwa uchukue uamuzi wa busara ili kelele za wananchi kuhusiana na tozo hizi ziweze kukoma.
Epuka sana washauri wabaya.