Vp kaka,
Ni vizuri sana kutafuta mawaidha kabla ya kufanya jambo, very wise.
Magari ya Mitsubishi ni magari mazuri mno, ukiangalia malori yao ya Fuso na pia Canter utaelewa ninacho sema.
'Tatizo' la hayo magari, na kwa kweli sio tatizo, ni kua hiyo sio Toyota! Nina maana gani hapa? Ukifanya uchunguzi mdogo tu wa kuzunguka mjini ukiangalia karakana zinazotoa huduma ya matengenezo kwa malori ya Fuso au Canter - magari ya Mitsubishi ambayo ni mengi humu na hayana usumbufu, utagundua Mitsubishi ndio tele pale na mafundi wana uzoefu na ujuzi mkubwa; ukiangazia upande wa matoleo yao ya magari madogo (iO, lancer, n.k.) utagundua sio mengi barabarani zetu, mafundi walioyazoea ni nadra kupata na kwa hivyo hata spare ni mtihani.
Hivi ni kusema magari haya hayafai huku kwetu? La hasha! Kwa kawaida chombo hakiharibiki katika matumizi yake ya kawaida - kwa uendeshaji kawaida kama ni gari, bali upata tu kuisha kwa baadhi ya vipuri - wear and tear! Matatizo uja pale unapoendelea kulitumia bila matunzo/maboresho/marekebisho, linapokarabatiwa kwa njia za mrengo(shortcut) ili kurudi barabarani tu, na pia pale fundi anpokosa kufata mbinu na maadili ya kiufundi.
Pole kwa taarifa ndeeefu, lakini issue ni ya muhimu na ni bora kuelewa vizuri. All the best should you go for the car.