Inaweza ikatosha kama utaanza na mahitaji muhimu na yanayotoka dukani haraka kwanza.Ndugu Habari za wakati huu.
awali yote napenda kuwajulia hali zenu mahali popote mlipo Tanzania na duniani kwa ujumla.
Mara baada ya salamu hii napenda kuwajulisha lengo la uzi huu.
Mimi ni muajiriwa serikalini kama mnavyojua hali ilivyo mishahara imegota no increment no ongezeko. Kama mtumishi mwenye weledi napenda kujiongeza kwa namna nyingine kuongeza kipato changu kwa kufanya biashara ya duka la mahitaji ya nyumbani n.k. Nimekopa mahala million 2 kwa ajili hiyo.
Hivyo kama mzoefu wewe unayesoma uzi huu naomba ushauri, je pesa hiyo itatosha kwa hili? Je vitu gani vya msingi kuzingatia ili kujikwamua na biashara hii. Nipo Makambako Njombe. Pia kama kuna ushauri mwingine Tafadhali naomba mnishauri nitatokaje?
Asanteni wote na pia nawatikia wakati mwema.
Asante kwa ushauri wako nduguInaweza ikatosha kama utaanza na mahitaji muhimu na yanayotoka dukani haraka kwanza.
Tenga pesa ya kodi ( angalau miezi sita), mzani, meza (simple tu) ya kuwekea mzani, (mahitaji mengine kama shelves za kuwekea bidhaa ndogondogo na mengineyo achana nayo kwanza)
Anza na bidhaa ambazo kila siku lazima zinunuliwe mfano unga,mchele,maharage,sukari,ngano n.k (kila bidhaa ukiwa na angalau 50kg sio mbaya). Faida utakayokua unapata utaongezea kwenye mtaji na duka litaanza kukua na kupanuka, kama umeoa ni vizur ukamuweka wife(kama ni jobless) akawa muuzaji ili ku-save pesa ya kumlipa muuzaji wa kukuuzia duka
Nashukuru kwa ushauriZingatia pia location ya biashara , kwa kuwa unaanza nakushauri tafuta sehem ambayo hamna maduka kabisa (hapa utakua umewasogezea huduma wateja hivyo hawatohangaika kwenda mbali kununua bidhaa). Pia jiandae kwa competition huko mbeleni, wabongo wana kawaida ya kucopy na kupaste idea pale wanapoona unanufaika sana
Kila la heriAsante kwa ushauri wako ndugu