econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,522
- 40,795
Kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, Nina ushauri Mmoja tu kwako. Naomba nikushauri ya kwamba tofautisha nafasi ya Uwaziri Mkuu na nafasi ya ukatibu mwenezi wa CCM.
Ushauri wangu ni kwamba Kuna kauli ambazo hutakiwi kuongea kwa nafasi uliyonayo ya Waziri Mkuu. Wewe ni kiranja wa Mawaziri wengine, inashangaza sana unapoongea jambo la ukakasi mbele ya umma.
Kwa mfano, Waziri Mkuu kusimama na kusema Kuna mtu alitumiwa billioni Tano kwenye Mpesa bila yeye kujua na kupewa maelekezo ni kauli ya uongo sana. Ni Mpesa Gani inaweza kupokea bilioni Tano kwa wakati Mmoja?. Na mpaka Leo huyo mtu hakuwahi kumatwa Wala kushtakiwa mahakamani.
Kwa Sasa una trend na kauli yako ya kwamba Kuna mtu mmemkamata amehaidiwa shilingi milioni mia akipeleka vijana kuuawa. Swali ni nani anayewaua hao vijana? Punguza hizi propaganda hazitakusaidia. Wewe ni Waziri Mkuu sio Katibu mwenezi wa CCM. Muachie propaganda Fares Burhani au Kenan Kihongosi.
Wewe ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo unwajibika kwa watanzania wote bila ubaguzi. Unapoleta propaganda ili kuwachafua wapinzani hasa CHADEMA unakosea sana. Ongea lugha za kuunganisha watu na kuleta watu pamoja. Kama Kuna shida Waite wenzako muongee sio kuchochea moto kwa kauli za uongo ambazo sio sahihi.
Nimalize kwa kusema unaboa sana na unakera sana kwa kauli zako, kama Kuna machafuko yatatokea wewe ndio utakuwa chanzo kwa kauli zako. Wananchi wametulia usiwachoche hasira zao kabisa. Hata October 29 watu waliingia mtaani baada ya kuona dhihaka za viongozi kama nyie. Kama utaendelea na ma propaganda yako hautafanikiwa utaanguka chini. Wako wapi akina ndugai, Tulia, Bashungwa waliojiona wamefika?. Tafakari sana.