Mhe. Rais ni raia namba moja katika nchi yetu ya Tanzania lazima apewe ulinzi na heshima yote pale anapopita. Juzi Mhe. Rais alikuwa na safari ya kwenda Dodoma lakini adha waliyopata wenye vyombo vya usafiri katika njia iendayo Dodoma ilikuwa ni adhabu tosha.
Magari yalianza kusimamishwa tangu asubuhi mpaka pale Mhe. Rais alipopita. Wengi walichelewa shughuli zao na wengine kupata usumbufu mkubwa. Ninashauri kuwa ikiwa Mhe. Rais anapita sehemu fulani basi vyombo vyote vya usafiri visimamishwe kabla ya nusu saa ili kumuwezesha Mhe. Rais aweze kupita kwa usalama kuliko juzi wakati vyombo vya usafiri vilisubiri mpaka masaa mawili na hata zaidi.
Nathibitisha hata Mhe. Rais asingependa wananchi wake wapate usumbufu wakati anapopita sehemu fulani.