Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ni wazi suala la kununua Dreamliner limetupiga sana, kwa kuwa tulitegemea zingepiga route za nje na kuingiza faida lakini mambo hayajawa hivyo. Na Corona imeharibu hata zaidi.
Ushauri wangu kwa raisi ajae, Tundu Lissu au Magufuli - uza hizo Dreamliner tuweke kipaombele kwenye flights za ndani tu. Achana na mambo ya kwenda Bombay au China, wakati muafaka ukifika tutafanya hivyo lakini kwa sasa ushindani ni mkubwa hata mashirika makubwa yanashindwa.
Lengo iwe kuifanya airport ya Dar kama stand ya mabasi ya mikoani inapofika asubuhi. Ndege zetu saizi ndogo ya Bombardier ziwe zimejipanga kwenda Arusha, Mwanza, Mbeya, Kigoma, Bukoba, Tabora, Mtwara Lindi nk, kila siku asubuhi, zikifanya ruti moja au mbili.
Na nauli lazima ishuke sana kiasi kwamba hata mwananchi wa kawaida aweze kumudu ili ndege ziwe zinaenda zimejaa abiria. Achana na mambo ya biskuti kwenye ndege, ndege ziwe zinafanya kazi katika mpangilio wa low cost airline. Weka baadhi ya nauli karibu sawa na nauli ya basi au juu kidigo ili ku-promote abiria kusafiri kwa ndege. Yaani tufanye kwa namna ya kupunguza kabisa mabasi barabarani.
Kama ukitaka route za nje sana sana weka route za East Afrika Community. Hata Joburg bondeni kule hamna haja ya kwenda.
Nawaambia tukifanya hivi tutafanikiwa sana!