Ushauri kwa Serikali: Ajira za mkataba ndiyo suluhisho pekee la uhaba wa ajira nchini

Wabongo tunajisahau sana kijana ukimpa mkataba wa miaka mitano anajisahau mpaka miaka mitano inaisha ndo anang’ang’ana anunue godoro
Akijisahau si inakula kwake na ataikumbuka hio hela akiwa kwenye msoto! Kusema serikali itoe hela bure bure hizo pesa hazitawafikia walengwa!
 
 
una mawazo mazuri ila umesahau hao unaotaka wastaafu mapema ndo wanaowatunza na kuwahudumia hao wanaotafuta ajira hadi wanafikia hatua ya kupata sifa za kuomba hizo ajira.

Kwa maneno mepesi iwapo wazo lako litatimia litafanya vijana wengi kuishia mtaani kwa kukosa sifa za kuajiriwa. wewe ushukuru umesomeshwa na kupata hizo sifa ila usiharibie wenzako wa baadae.
 
haya basi chukua pointi tatu mkuu!!!
 
kwa hio kila baada ya miaka mitano serikal ianze tena kuwafubdisha maana walr wenye uzoefu watakua wamesitishiwa mkataba.idea yako is pointress
 
Wazo ni zuri ila haliwezi kutekelezeka kwasababu ya sera mbovu ya ajira na hali ya kiuchumi ya sekta nyingi za ajira.Ili kutekeleza hilo inabidi kwanza nchi iwe na sera ya uchumi imara inayoeleweka kuanzia kwenye sekta rasmi hadi binafsi.Pia elimu ya vyuo vyetu ifanyiwe mabadiliko makubwa ili kupatikane watu compitent wakuingia moja kwa moja kazini bila kuhitaji miaka ya uzoefu kitu ambacho kwa hapa bongo bado ni mtihani,Kufanya maboresho ya msingi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.Lakini pia kurekebisha sheria za ajira ili kuendana na hali na mazingira.Hapo kwa wsnasiasa ni sawa kabisa maana wao hakuhitajiki uzoefu wowote.miaka mitano mitano inawatosga kabisa.
 
Haya tumeyasema mda mkuu, hakuna sababu serikali kutoa ajira za maisha kwa watumishi wkt kuna lundo la watu wenye sifa mtaani, waweke ajira za mikataba serikalini na kwamba wale the best wawe wanaongezewa mikataba, iwe mkataba wa miaka mitano tu, hapo mtu anatoka anaingia mwengine, yule aliyetoka anakuwa tayari ameshakuwa expert anayeweza kujitafutia maisha sehemu nyingine, lkn pia anakuwa tayari na mtaji wa kutosha incase inatokea anakosa pa kujishikiza anakuwa anafanya mambo yake.


Hii itasaidia kurudisha nidhamu kwa watumishi kwani mtu atajituma ili apate kuongezewa mkataba, lkn pia itafanya watumishi wawe makini na matumizi ya hovyo cz watajipanga mapema kuliko kumuacha mtu amejisahau kazini matokeo yake anastaafu akiwa hana kitu.
 
Hakuna haja ya kulipana mishahara mikubwa, hii hii inatosha na watu watajipanga mapema, hakuna pesa inayotosha isipokuwa ni nidhamu ya pesa tu, mtu akilipwa one milion huku akijua miaka mitano hana chake basi hyo one milion itafanya mengi kuliko ilivyo sasa.
 
Kuendesha ajira za mkataba itakuwa gharama kubwa kwa serikali na sidhani kama wanafikiria hilo.....pia itakuwa mtihani kwenye kujenga uzoefu wa watumishi ambao watatakiwa kuongoza idara na taasisi.
 
Uongo..

Kwa miaka 8 basi tayari mfumo unaoshauri unakutaka ujiajiri...
Haya jiajiri kama unavyoshauri
 
Uongo..

Kwa miaka 8 basi tayari mfumo unaoshauri unakutaka ujiajiri...
Haya jiajiri kama unavyoshauri

Umenichekesha Kate, wanaongea kama vile kila mtu anaweza kujiajiri,,,,,mwingine Anadai Fresh graduates hawawezi kujiajiri watashindwa sasa mtu unajiuliza baada ya Miaka mitano ndani ya office huyu graduate ambae mwanzo alikua hajui kujiajiri anakua transformed baada ya miaka 5 na kujua kujiajiri, The question is HOW? watuambie labda tutaweza kufika muafaka
 
Wanadai issue ni kipato/mtaji
 
Atleast ataachwa na kitu mkononi! Knowing thats your last bullet in hand itampa ujasiri wa kujaribu mishe kadhaa maana mtaji anao.

Kuisha kwa mkataba ukiwa na 70M mkononi inaweza kuwa sawa na kukabidhiwa cheti cha degree bila sent 5 kisha uambiwe jiajiri?
 
kwa hio kila baada ya miaka mitano serikal ianze tena kuwafubdisha maana walr wenye uzoefu watakua wamesitishiwa mkataba.idea yako is pointress
Training inachukuaga miaka mitano kwani? Probation si huwa miezi mitatu mpaka 6!

Mbona mnaongea kama vile majuha?
 
Yaani baada ya kila miaka 5 watu wapya kazini
Huko kazini kutakua mchaka mchaka watu ni kuwaza kufanikisha mambo yao tu ubunifu utakua hakuna
Kwani hio miaka 60 kuna ambaye hawazii mambo yake binafsi? Wengi si wapigaji tu tena ubaya wa hii miaka 60 mtu akishapata mkataba wa Utumishi tu ana relax maana anajua follow ups huwa sio rahisi na kufukuzwa ni ngumu serikalini hata akivurunda! Ndio maana mtu yupo radhi aache mshahara wa million private company akimbilie laki 8 ya serikalini😅
 
Ndio maana naipenda JF.
 
We unaonekana unamenya serikalini wewe ndio maana hutamani ajira yako ikatishwe kwa mkataba! Mi nina hakika 80% ya waajiriwa ikatokea waambiwe ajira basi imetosha mpishe wengine basi kuna wengi tutawazika kwa presha.

Ugumu wakujiajiri uko pale pale ila utofauti utakuwa kwamba mwenye mtaji mkubwa ana chance kubwa yakutoboa mfano wewe umemeki 70M! Ukianza biashara ya 2M ikaanguka, ukarudia tena ikaanguka mpaka itakapokubali kuwork out you stand a chance by far!

Imagine graduate kafanya the same kwa 2M tu biashara imemkataa! Hela imepoteaa anarudishaje tumaini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…