SoC01 Ushauri kwa Serikali kuhusu jinsi ya kukabiliana na tozo kubwa za miamala

SoC01 Ushauri kwa Serikali kuhusu jinsi ya kukabiliana na tozo kubwa za miamala

Stories of Change - 2021 Competition

Ngomamalick

New Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Ushauri wangu kwa Serikali kukabiliana na tozo la kodi kuwa kubwa na makato kwa wananchi na kutotegemea kwenye miamala ya fedha tu

Serikali ingetazama namna ya kuwaokoa wananchi kwenye wimbi hili Ili pia kuongeza mapato na kuacha kutegemea sehemu moja kwenye ukusanyaji wa kodi
Kwa kufanya yafuatayo.

1. Kuongeza na na kuboresha maeneo mbalimbali nchini ambayo ni sehemu ya utalii ili kuweza kukusanya Fedha za kutosha katika sekta hii ya utalii kama kuongeza ufanisi wa utunzaji wa mazingira na wanyamapori wasipotee na na pia kuboresha miundombinu mbalimbali ili kuweza kuhakikisha ubora wa huduma za watalii

2. Kutoa elimu juu ya kilimo bora kwa wananchi chenye tija Aina ya mazao ya kulima na misimu ya kulima na namna ya kulima mazao hayo na namna ya kuyalinda na magonjwa,kiangazi ili watu wazalishe mazao bora yaweze kua na ushindani katika soko la nnje na ndani.

3. Kupunguza bei katika pembejeo za kilimo na uvuvi ili watu waweze kujihusisha na kilimo bora na uvuvi kuweza kuhakikisha uwepo wa mazao ya chakula na biashara na mauzo yakiongezeka pia ukusanyaji wa kodi Utakua mkubwa

4.Kutoa elimu katika ngazi zote za elimu na kutoa mitaji kama mikopo na usimamizi kwa wananchi juu ya ujasiriamali na kujitegemea ili kupunguza wimbi la kukosekana kwa ajila na watu wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara ukusanyaji wa kodi Utakua mkubwa na pessa itapatikana

5. Kutoa usimamizi elimu,na Fedha kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wakati ili kushawishi na kuwezesha shughuli nyingi za ujasiriamali na upatikanaji wakodi Utakua mkubwa

6. Kukusanya makato ya ambayo wananchi wanaya mudu ili kuepusha ukwepaji wa kulipa kodi na uchimbaji mzuri wa madini na jinsi ya kuchakata mpaka Bidhaa ya mwinsho ambayo ni madini kuepuka kuuza makinikia nnje ya nnchi na kupata stahiki kutokana na Kiasi cha madini kilichotoka na kukwepa wizi wa madini

7. Kuboresha viwanda na pia kutafuta tekinolojia kutoka nnchi jirani kupunguza uingizaji wa bidhaa za kigeni ili kukuza matumizi ya teknolojia yetu na kutoa ajira kwa vijana na kushusha bei ya bidhaa zinazotoka nnje ya nnchi ili kutoa soko kwa bidhaa za ndani hii itasaidia uchumi kukua kwa kiasi kikubwa.

8. Kukuza uwekezaji na kutoa fursa kwa kuwapa mazingira bora wawekezaji kutoka Tanzania na watu wa nje ya nchi ili kuweza kuruhusu Upatikanaji wa ajira kwa wananchi na upatikanaji wa bidhaa za kutosha kwa jamii ,hii itapunguza uwepo wa watu wasio ajiriwa na tegemezi kwa serikali hivyo mzunguko wa pesa Utakua mkubwa

9. Kuboresha huduma za kiafya kwa mama ,watoto,na walemavu ili kupunguza vifo na uambukizaji wa magonjwa na kupata nguvukazi ambayo itaweza kufanya kazi kwa nguvu zote katika jamii na kufanya mzunguko wa pesa uwepo kwa hali ya juu maana mtaji mkuu ni Afya

10. Kuboresha miundombinu kama umeme,majisafi,Barabara vijijini na mijini ili kuweza kuruhusu usafirishaji wa bidhaa na watu katika maeneo mbalimbali ya nchi na kurahisisha ujengaji wa viwanda hivyo kurahisisha huduma za kijamii kuwafikia watu kwa urahisi na kufanya watu waweze kufanya kazi kwabidii ili kujiingizia kipato.

11. Kuboresha demokrasia ya chi ili kuleta Amani mshikamano na ufanyaji kazi kwa mshikamano baina ya watumishi na wananchi hii itarahisisha hata viongozi kupata matatizo ya viongozi wao kwa wepesi na kuleta maendeleo katika jamii na kurahisisha ukusanyaji wa kodi .
 
Upvote 3
Safi mkuu.. ila jitahidi kuhakiki andiko lako zaidi kabla ya kulipost maana kuna maneno mengine hayako sahihi.. tembelea na kwangu pia kwako nimevote
 
Back
Top Bottom